إِنَّكَ إِن تَذَرۡهُمۡ يُضِلُّواْ عِبَادَكَ وَلَا يَلِدُوٓاْ إِلَّا فَاجِرٗا كَفَّارٗا
Hakika ukiwaacha watawapoteza waja wako, wala wao hawatazaa ila waovu makafiri.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Hao ukiwaacha, bila kuwaangamiza, watawapoteza waja wako waliokuamini na kuwapotosha njia ya haki, na haji yoyote kutokana na migongo yao na vizazi vyao isipokuwa yule aliyepotoka na njia ya haki na kukukanusha wewe sana na kukuasi.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس