Sura Al-Infitar kwa Kiswahili
سورة الإنفطار · Aya: 19 · Makka
Tafsiri: Ali Muhsin Al - Swahili translation
-
1
إِذَا ٱلسَّمَآءُ ٱنفَطَرَتۡ
Al-Infitar
Mbingu itapo chanika, -
2
وَإِذَا ٱلۡكَوَاكِبُ ٱنتَثَرَتۡ
Na nyota zitapo tawanyika, -
3
وَإِذَا ٱلۡبِحَارُ فُجِّرَتۡ
Na bahari zitakapo pasuliwa, -
4
وَإِذَا ٱلۡقُبُورُ بُعۡثِرَتۡ
Na makaburi yatapo fukuliwa, -
5
عَلِمَتۡ نَفۡسࣱ مَّا قَدَّمَتۡ وَأَخَّرَتۡ
Hapo kila nafsi itajua ilicho tanguliza, na ilicho bakisha nyuma. -
6
يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡإِنسَٰنُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ ٱلۡكَرِيمِ
Ewe mwanaadamu! Nini kilicho kughuri ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu? -
7
ٱلَّذِي خَلَقَكَ فَسَوَّىٰكَ فَعَدَلَكَ
Aliye kuumba, akakuweka sawa, akakunyoosha, -
8
فِيٓ أَيِّ صُورَةࣲ مَّا شَآءَ رَكَّبَكَ
Katika sura yoyote aliyo ipenda akakujenga. -
9
كَلَّا بَلۡ تُكَذِّبُونَ بِٱلدِّينِ
Sivyo hivyo! Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Malipo. -
10
وَإِنَّ عَلَيۡكُمۡ لَحَٰفِظِينَ
Na hakika bila ya shaka wapo walinzi juu yenu, -
11
كِرَامࣰا كَٰتِبِينَ
Waandishi wenye hishima, -
12
يَعۡلَمُونَ مَا تَفۡعَلُونَ
Wanayajua mnayo yatenda. -
13
إِنَّ ٱلۡأَبۡرَارَ لَفِي نَعِيمࣲ
Hakika wema bila ya shaka watakuwa katika neema, -
14
وَإِنَّ ٱلۡفُجَّارَ لَفِي جَحِيمࣲ
Na hakika waovu bila ya shaka watakuwa Motoni; -
15
يَصۡلَوۡنَهَا يَوۡمَ ٱلدِّينِ
Wataingia humo Siku ya Malipo. -
16
وَمَا هُمۡ عَنۡهَا بِغَآئِبِينَ
Na hawatoacha kuwamo humo. -
17
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا يَوۡمُ ٱلدِّينِ
Na nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani? -
18
ثُمَّ مَآ أَدۡرَىٰكَ مَا يَوۡمُ ٱلدِّينِ
Tena nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani? -
19
يَوۡمَ لَا تَمۡلِكُ نَفۡسࣱ لِّنَفۡسࣲ شَيۡـࣰٔاۖ وَٱلۡأَمۡرُ يَوۡمَئِذࣲ لِّلَّهِ
Siku ambayo nafsi haitakuwa na madaraka yoyote juu ya nafsi; na amri yote siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu tu.