Sura Al-Mutaffifin kwa Kiswahili
سورة المطففين · Aya: 36 · Makka
Tafsiri: Ali Muhsin Al - Swahili translation
-
1
وَيۡلࣱ لِّلۡمُطَفِّفِينَ
Al-Mutaffifin
Ole wao hao wapunjao! -
2
ٱلَّذِينَ إِذَا ٱكۡتَالُواْ عَلَى ٱلنَّاسِ يَسۡتَوۡفُونَ
Ambao wanapo jipimia kwa watu hudai watimiziwe. -
3
وَإِذَا كَالُوهُمۡ أَو وَّزَنُوهُمۡ يُخۡسِرُونَ
Na wao wanapo wapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza. -
4
أَلَا يَظُنُّ أُوْلَٰٓئِكَ أَنَّهُم مَّبۡعُوثُونَ
Kwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa -
5
لِيَوۡمٍ عَظِيمࣲ
Katika Siku iliyo kuu, -
6
يَوۡمَ يَقُومُ ٱلنَّاسُ لِرَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Siku watapo msimamia watu Mola Mlezi wa walimwengu wote? -
7
كَلَّآ إِنَّ كِتَٰبَ ٱلۡفُجَّارِ لَفِي سِجِّينࣲ
Hasha! Hakika maandiko ya wakosefu bila ya shaka yamo katika Sijjin. -
8
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا سِجِّينࣱ
Unajua nini Sijjin? -
9
كِتَٰبࣱ مَّرۡقُومࣱ
Kitabu kilicho andikwa. -
10
وَيۡلࣱ يَوۡمَئِذࣲ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo kwa wanao kadhibisha! -
11
ٱلَّذِينَ يُكَذِّبُونَ بِيَوۡمِ ٱلدِّينِ
Ambao wanaikadhibisha Siku ya Malipo. -
12
وَمَا يُكَذِّبُ بِهِۦٓ إِلَّا كُلُّ مُعۡتَدٍ أَثِيمٍ
Wala haikadhibishi ila kila mwenye kuruka mipaka, mwenye dhambi. -
13
إِذَا تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِ ءَايَٰتُنَا قَالَ أَسَٰطِيرُ ٱلۡأَوَّلِينَ
Anapo somewa Aya zetu husema: Ni visa vya watu wa kale! -
14
كَلَّاۖ بَلۡۜ رَانَ عَلَىٰ قُلُوبِهِم مَّا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ
Hasha! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao hao walio kuwa wakiyachuma. -
15
كَلَّآ إِنَّهُمۡ عَن رَّبِّهِمۡ يَوۡمَئِذࣲ لَّمَحۡجُوبُونَ
Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa na neema za Mola wao Mlezi. -
16
ثُمَّ إِنَّهُمۡ لَصَالُواْ ٱلۡجَحِيمِ
Kisha wataingia Motoni! -
17
ثُمَّ يُقَالُ هَٰذَا ٱلَّذِي كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ
Kisha waambiwe: Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyakadhabisha. -
18
كَلَّآ إِنَّ كِتَٰبَ ٱلۡأَبۡرَارِ لَفِي عِلِّيِّينَ
Hasha! Hakika maandiko ya watu wema bila ya shaka yamo katika I'liyyin. -
19
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا عِلِّيُّونَ
Na nini kitakacho kujuvya nini I'liyyin? -
20
كِتَٰبࣱ مَّرۡقُومࣱ
Kitabu kilicho andikwa. -
21
يَشۡهَدُهُ ٱلۡمُقَرَّبُونَ
Wanakishuhudia walio karibishwa. -
22
إِنَّ ٱلۡأَبۡرَارَ لَفِي نَعِيمٍ
Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema. -
23
عَلَى ٱلۡأَرَآئِكِ يَنظُرُونَ
Wakae juu ya viti vya enzi wakiangalia. -
24
تَعۡرِفُ فِي وُجُوهِهِمۡ نَضۡرَةَ ٱلنَّعِيمِ
Utatambua katika nyuso zao mng'aro wa neema, -
25
يُسۡقَوۡنَ مِن رَّحِيقࣲ مَّخۡتُومٍ
Watanyweshwa kinywaji safi kiliyo tiwa muhuri, -
26
خِتَٰمُهُۥ مِسۡكࣱۚ وَفِي ذَٰلِكَ فَلۡيَتَنَافَسِ ٱلۡمُتَنَٰفِسُونَ
Muhuri wake ni miski. Na katika hayo washindanie wenye kushindana. -
27
وَمِزَاجُهُۥ مِن تَسۡنِيمٍ
Na mchanganyiko wake ni Tasniim, -
28
عَيۡنࣰا يَشۡرَبُ بِهَا ٱلۡمُقَرَّبُونَ
Chemchem watakayo inywa walio kurubishwa. -
29
إِنَّ ٱلَّذِينَ أَجۡرَمُواْ كَانُواْ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ يَضۡحَكُونَ
Kwa hakika wale walio kuwa wakosefu walikuwa wakiwacheka walio amini. -
30
وَإِذَا مَرُّواْ بِهِمۡ يَتَغَامَزُونَ
Na wanapo pita karibu yao wakikonyezana. -
31
وَإِذَا ٱنقَلَبُوٓاْ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِمُ ٱنقَلَبُواْ فَكِهِينَ
Na wanapo rudi kwa watu wao hurudi nao wamefurahi. -
32
وَإِذَا رَأَوۡهُمۡ قَالُوٓاْ إِنَّ هَٰٓؤُلَآءِ لَضَآلُّونَ
Na wanapo waona husema: Hakika hawa ndio khasa walio potea. -
33
وَمَآ أُرۡسِلُواْ عَلَيۡهِمۡ حَٰفِظِينَ
Na wao hawakutumwa wawe walinzi juu yao. -
34
فَٱلۡيَوۡمَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مِنَ ٱلۡكُفَّارِ يَضۡحَكُونَ
Basi leo walio amini ndio watawacheka makafiri, -
35
عَلَى ٱلۡأَرَآئِكِ يَنظُرُونَ
Nao wako juu ya viti vya enzi wakiangalia. -
36
هَلۡ ثُوِّبَ ٱلۡكُفَّارُ مَا كَانُواْ يَفۡعَلُونَ
Je! makafiri wamelipwa malipo ya yale waliyo kuwa wakiyatenda?