يُرِيدُونَ أَن يَخۡرُجُواْ مِنَ ٱلنَّارِ وَمَا هُم بِخَٰرِجِينَ مِنۡهَاۖ وَلَهُمۡ عَذَابٞ مُّقِيمٞ
Watataka watoke Motoni, lakini hawatatoka humo, na watakuwa na adhabu inayo dumu.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Makafiri hawa watataka watoke Motoni kwa ajili ya visanga vyake wanavyovipata, lakini hawatakuwa na njia yoyote ya kufanya hivyo. Na watakuwa na adhabu ya kudumu.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس