ترجمة سورة التين

الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
ترجمة معاني سورة التين باللغة السواحلية من كتاب الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس .

Mwenyezi Mungu Anaapa kwa tini na zaituni, nayo ni miongoni mwa matunda yanayojulikana.
Na Anaapa kwa jabali la Ṭūr Sīnā’ ambalo Mwenyezi Mungu Alisema na Mūsā juu yake.
Na Anaapa kwa Mji huu wa amani, usiokuwa na mambo ya kutisha. Nao ni mji wa Makkah, chimbuko la Uislamu.
Hakika Tumemuumba binadamu katika sura nzuri.
Kisha Tutampeleka Motoni akiwa hakumtii Mweyezi Mungu na hakuwafuata Mitume.
Isipokuwa wale walioamini na wakafanya amali njema; wao watakuwa na malipo makubwa yasiyokatika wala kupungua.
Ni lipi linalokupelekea wewe, ewe binadamu, kukanusha kufufuliwa na kulipwa, hali ya kuwa kuna dalili wazi kwamba Mwenyezi Mungu Ana uweza wa kufanya hayo?
Je, Hakuwa Mwenyezi Mungu , Ambaye Ameiweka Siku hii kutoa uamuzi baina ya watu, ni muadilifu zaidi ya wanaosifika kuwa ni waadilifu katika kila Alichokiumba? Kwani? Alikuwa. Basi wataachwa viumbe rebe: hawaamrishwi wala hawakatazwi wala hawalipwi kwa mema wala hawateswi kwa mabaya? Hilo si sahihi wala haliwi.
Icon