Sura Al-A'la kwa Kiswahili
Al'A'alah · سورة الأعلى · Aya: 19 · Makka
Tafsiri: Ali Muhsin Al - Swahili translation
-
1
سَبِّحِ ٱسۡمَ رَبِّكَ ٱلۡأَعۡلَى
Al'A'alah
Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa, -
2
ٱلَّذِي خَلَقَ فَسَوَّىٰ
Aliye umba, na akaweka sawa, -
3
وَٱلَّذِي قَدَّرَ فَهَدَىٰ
Na ambaye amekadiria na akaongoa, -
4
وَٱلَّذِيٓ أَخۡرَجَ ٱلۡمَرۡعَىٰ
Na aliye otesha malisho, -
5
فَجَعَلَهُۥ غُثَآءً أَحۡوَىٰ
Kisha akayafanya makavu, meusi. -
6
سَنُقۡرِئُكَ فَلَا تَنسَىٰٓ
Tutakusomesha wala hutasahau, -
7
إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُۚ إِنَّهُۥ يَعۡلَمُ ٱلۡجَهۡرَ وَمَا يَخۡفَىٰ
Ila akipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhaahiri na yaliyo fichikana. -
8
وَنُيَسِّرُكَ لِلۡيُسۡرَىٰ
Na tutakusahilishia yawe mepesi. -
9
فَذَكِّرۡ إِن نَّفَعَتِ ٱلذِّكۡرَىٰ
Basi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa. -
10
سَيَذَّكَّرُ مَن يَخۡشَىٰ
Atakumbuka mwenye kuogopa. -
11
وَيَتَجَنَّبُهَا ٱلۡأَشۡقَى
Na atajitenga mbali nayo mpotovu, -
12
ٱلَّذِي يَصۡلَى ٱلنَّارَ ٱلۡكُبۡرَىٰ
Ambaye atauingia Moto mkubwa. -
13
ثُمَّ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحۡيَىٰ
Tena humo hatakufa wala hawi hai. -
14
قَدۡ أَفۡلَحَ مَن تَزَكَّىٰ
Hakika amekwisha fanikiwa aliye jitakasa. -
15
وَذَكَرَ ٱسۡمَ رَبِّهِۦ فَصَلَّىٰ
Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akasali. -
16
بَلۡ تُؤۡثِرُونَ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا
Lakini nyinyi mnakhiari maisha ya dunia! -
17
وَٱلۡأٓخِرَةُ خَيۡرࣱ وَأَبۡقَىٰٓ
Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi. -
18
إِنَّ هَٰذَا لَفِي ٱلصُّحُفِ ٱلۡأُولَىٰ
Hakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo, -
19
صُحُفِ إِبۡرَٰهِيمَ وَمُوسَىٰ
Vitabu vya Ibrahimu na Musa.