Sura 'Abasa kwa Kiswahili
Abasa · سورة عبس · Aya: 42 · Makka
Tafsiri: Ali Muhsin Al - Swahili translation
-
1
عَبَسَ وَتَوَلَّىٰٓ
Abasa
Alikunja kipaji na akageuka, -
2
أَن جَآءَهُ ٱلۡأَعۡمَىٰ
Kwa sababu alimjia kipofu! -
3
وَمَا يُدۡرِيكَ لَعَلَّهُۥ يَزَّكَّىٰٓ
Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika? -
4
أَوۡ يَذَّكَّرُ فَتَنفَعَهُ ٱلذِّكۡرَىٰٓ
Au atawaidhika, na mawaidha yamfae? -
5
أَمَّا مَنِ ٱسۡتَغۡنَىٰ
Ama ajionaye hana haja, -
6
فَأَنتَ لَهُۥ تَصَدَّىٰ
Wewe ndio unamshughulikia? -
7
وَمَا عَلَيۡكَ أَلَّا يَزَّكَّىٰ
Na si juu yako kama hakutakasika. -
8
وَأَمَّا مَن جَآءَكَ يَسۡعَىٰ
Ama anaye kujia kwa juhudi, -
9
وَهُوَ يَخۡشَىٰ
Naye anaogopa, -
10
فَأَنتَ عَنۡهُ تَلَهَّىٰ
Ndio wewe unampuuza? -
11
كَلَّآ إِنَّهَا تَذۡكِرَةࣱ
Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana. -
12
فَمَن شَآءَ ذَكَرَهُۥ
Basi anaye penda akumbuke. -
13
فِي صُحُفࣲ مُّكَرَّمَةࣲ
Yamo katika kurasa zilizo hishimiwa, -
14
مَّرۡفُوعَةࣲ مُّطَهَّرَةِۭ
Zilizo inuliwa, zilizo takaswa. -
15
بِأَيۡدِي سَفَرَةࣲ
Zimo mikononi mwa Malaika waandishi, -
16
كِرَامِۭ بَرَرَةࣲ
Watukufu, wema. -
17
قُتِلَ ٱلۡإِنسَٰنُ مَآ أَكۡفَرَهُۥ
Ameangamia mwanaadamu! Nini kinacho mkufurisha? -
18
مِنۡ أَيِّ شَيۡءٍ خَلَقَهُۥ
Kwa kitu gani amemuumba? -
19
مِن نُّطۡفَةٍ خَلَقَهُۥ فَقَدَّرَهُۥ
Kwa tone la manii, akamuumba na akamkadiria. -
20
ثُمَّ ٱلسَّبِيلَ يَسَّرَهُۥ
Kisha akamsahilishia njia. -
21
ثُمَّ أَمَاتَهُۥ فَأَقۡبَرَهُۥ
Kisha akamfisha, akamtia kaburini. -
22
ثُمَّ إِذَا شَآءَ أَنشَرَهُۥ
Kisha apendapo atamfufua. -
23
كَلَّا لَمَّا يَقۡضِ مَآ أَمَرَهُۥ
La! Hajamaliza aliyo muamuru. -
24
فَلۡيَنظُرِ ٱلۡإِنسَٰنُ إِلَىٰ طَعَامِهِۦٓ
Hebu mtu na atazame chakula chake. -
25
أَنَّا صَبَبۡنَا ٱلۡمَآءَ صَبࣰّا
Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu, -
26
ثُمَّ شَقَقۡنَا ٱلۡأَرۡضَ شَقࣰّا
Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu, -
27
فَأَنۢبَتۡنَا فِيهَا حَبࣰّا
Kisha tukaotesha humo nafaka, -
28
وَعِنَبࣰا وَقَضۡبࣰا
Na zabibu, na mimea ya majani, -
29
وَزَيۡتُونࣰا وَنَخۡلࣰا
Na mizaituni, na mitende, -
30
وَحَدَآئِقَ غُلۡبࣰا
Na bustani zenye miti iliyo songana baraabara, -
31
وَفَٰكِهَةࣰ وَأَبࣰّا
Na matunda, na malisho ya wanyama; -
32
مَّتَٰعࣰا لَّكُمۡ وَلِأَنۡعَٰمِكُمۡ
Kwa manufaa yenu na mifugo yenu. -
33
فَإِذَا جَآءَتِ ٱلصَّآخَّةُ
Basi utakapo kuja ukelele, -
34
يَوۡمَ يَفِرُّ ٱلۡمَرۡءُ مِنۡ أَخِيهِ
Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye, -
35
وَأُمِّهِۦ وَأَبِيهِ
Na mamaye na babaye, -
36
وَصَٰحِبَتِهِۦ وَبَنِيهِ
Na mkewe na wanawe - -
37
لِكُلِّ ٱمۡرِيࣲٕ مِّنۡهُمۡ يَوۡمَئِذࣲ شَأۡنࣱ يُغۡنِيهِ
Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha. -
38
وُجُوهࣱ يَوۡمَئِذࣲ مُّسۡفِرَةࣱ
Siku hiyo ziko nyuso zitazo nawiri, -
39
ضَاحِكَةࣱ مُّسۡتَبۡشِرَةࣱ
Zitacheka, zitachangamka; -
40
وَوُجُوهࣱ يَوۡمَئِذٍ عَلَيۡهَا غَبَرَةࣱ
Na nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi, -
41
تَرۡهَقُهَا قَتَرَةٌ
Giza totoro litazifunika, -
42
أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡكَفَرَةُ ٱلۡفَجَرَةُ
Hao ndio makafiri watenda maovu.