Sura Al-'Alaq kwa Kiswahili
Al'Alak · سورة العلق · Aya: 19 · Makka
Tafsiri: Ali Muhsin Al - Swahili translation
-
1
ٱقۡرَأۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلَّذِي خَلَقَ
Al'Alak
Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba, -
2
خَلَقَ ٱلۡإِنسَٰنَ مِنۡ عَلَقٍ
Amemuumba binaadamu kwa tone la damu, -
3
ٱقۡرَأۡ وَرَبُّكَ ٱلۡأَكۡرَمُ
Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote! -
4
ٱلَّذِي عَلَّمَ بِٱلۡقَلَمِ
Ambaye amefundisha kwa kalamu. -
5
عَلَّمَ ٱلۡإِنسَٰنَ مَا لَمۡ يَعۡلَمۡ
Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui. -
6
كَلَّآ إِنَّ ٱلۡإِنسَٰنَ لَيَطۡغَىٰٓ
Kwani! Hakika mtu bila ya shaka huwa jeuri -
7
أَن رَّءَاهُ ٱسۡتَغۡنَىٰٓ
Akijiona katajirika. -
8
إِنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ ٱلرُّجۡعَىٰٓ
Hakika kwa Mola wako Mlezi ndio marejeo. -
9
أَرَءَيۡتَ ٱلَّذِي يَنۡهَىٰ
Umemwona yule anaye mkataza -
10
عَبۡدًا إِذَا صَلَّىٰٓ
Mja anapo sali? -
11
أَرَءَيۡتَ إِن كَانَ عَلَى ٱلۡهُدَىٰٓ
Umeona kama yeye yuko juu ya uwongofu? -
12
أَوۡ أَمَرَ بِٱلتَّقۡوَىٰٓ
Au anaamrisha uchamngu? -
13
أَرَءَيۡتَ إِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰٓ
Umeona kama yeye akikanusha na anarudi nyuma? -
14
أَلَمۡ يَعۡلَم بِأَنَّ ٱللَّهَ يَرَىٰ
Hajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anaona? -
15
كَلَّا لَئِن لَّمۡ يَنتَهِ لَنَسۡفَعَۢا بِٱلنَّاصِيَةِ
Kwani! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele! -
16
نَاصِيَةࣲ كَٰذِبَةٍ خَاطِئَةࣲ
Shungi la uwongo, lenye makosa! -
17
فَلۡيَدۡعُ نَادِيَهُۥ
Basi na awaite wenzake! -
18
سَنَدۡعُ ٱلزَّبَانِيَةَ
Nasi tutawaita Mazabania! -
19
كَلَّا لَا تُطِعۡهُ وَٱسۡجُدۡۤ وَٱقۡتَرِب۩
Hasha! Usimt'ii! Nawe sujudu na ujongee!