وَأُحِيطَ بِثَمَرِهِۦ فَأَصۡبَحَ يُقَلِّبُ كَفَّيۡهِ عَلَىٰ مَآ أَنفَقَ فِيهَا وَهِيَ خَاوِيَةٌ عَلَىٰ عُرُوشِهَا وَيَقُولُ يَٰلَيۡتَنِي لَمۡ أُشۡرِكۡ بِرَبِّيٓ أَحَدٗا
Yakateketezwa matunda yake, akabaki akipindua pindua viganja vyake, kwa vile alivyo yagharimia, na miti imebwagika juu ya chanja zake. Akawa anasema: Laiti nisingeli mshiriki Mola wangu Mlezi na yeyote!
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Yakawa ni kweli yale maneno ya yule Muumini, na shamba likaharibika na vilivyomo ndani vikaangamia, akawa yule kafiri anageuza vitanga vyake vya mikono huku na huku kwa kulilia hasara na majuto kwa gharama aliyoitoa pale, na hali mitiyake imeanguka chini baadhi yake iko juu ya mingine, na akawa yuwasema, «Natamani lau nilizitambua neema za Mwenyezi Mungu na uweza Wake na sikumshirikisha Mwenyezi Mungu na yoyote.» Na haya ni majuto yake wakati ambapo majuto hayamfalii kitu.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس