قُلۡ سِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَٱنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلُۚ كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّشۡرِكِينَ
Sema: Safirini duniani muangalie ulikuwaje mwisho wa walio tangulia. Wengi wao walikuwa washirikina.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Sema, ewe Mtume, kuwaambia wenye kuyakanusha uliyokuja nayo, «Tembeeni kwenye sehemu za ardhi matembezi ya kuzingatia na kutia mambo akilini, na mtazame vile ulivyokuwa mwisho wa ummah waliopita wenye kukanusha, kama vile watu wa Nūḥ, ‘Ād na Thamūd, mtakuta kwamba mwisho wao walioishia ulikuwa mbaya zaidi na kikomo hiko walichokomea kilikuwa kibaya zaidi, kwani wengi wao walikuwa ni wenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس