أَوَلَمۡ يَتَفَكَّرُواْ فِيٓ أَنفُسِهِمۗ مَّا خَلَقَ ٱللَّهُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَمَا بَيۡنَهُمَآ إِلَّا بِٱلۡحَقِّ وَأَجَلٖ مُّسَمّٗىۗ وَإِنَّ كَثِيرٗا مِّنَ ٱلنَّاسِ بِلِقَآيِٕ رَبِّهِمۡ لَكَٰفِرُونَ
Je! Hawajifikirii nafsi zao? Mwenyezi Mungu hakuumba mbingu na ardhi na viliomo ndani yake ila kwa Haki na kwa muda maalumu. Na hakika watu wengi bila ya shaka ni wenye kukataa kuwa watakutana na Mola wao Mlezi.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Kwani hawakufikiri, hawa wakanushaji Mitume wa Mwenyezi Mungu na kukutana na Yeye, vile Mwenyezi Mungu Alivyowaumba, na kuwa wao Amewaumba na hawakuwa kitu chochote? Mwenyezi Mungu hakuumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake isipokuwa ni kwa ajili ya kusimamisha uadilifu, malipo mema na mateso na kutolea ushahidi upweke Wake na uweza Wake. Na kwa muda uliotajwa wa kukomea kwake nao ni Siku ya Kiyama. Na kwa hakika, wengi wa watu ni wenye kukataa na kukanusha kwa ujinga wao wa kutojua kuwa marejeo yao ni kwa Mwenyezi Mungu baada ya kutoweka kwao na kwa kughafilika kwao na Akhera.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس