ﯚ
surah.translation
.
ﰡ
ﭑ
ﰀ
«Ḥā, Mīm» Yametangulia maelezo kuhusu herufi zilizokatwa na kutengwa katika mwanzo wa sura ya Al-Baqarah.
Hii Qur’ani imeteremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Aliye Mshindi katika kuwatesa maadui Zake, Mwingi wa hekima katika uendeshaji wa mambo ya viumbe Vyake.
Hakika kwenye mbingu saba na ardhi ambapo humo viumbe vinatoka, na vilivyomo baina ya hivyo viwili miongoni mwa viumbe wa jinsi tofauti na aina mbalimbali, kuna dalili na hoja kwa wenye kuziamini.
Na katika kuwaumba nyinyi, enyi watu, na uumbaji wa vilivyotapakaa ardhini miongoni mwa vinavyotambaa juu yake, kuna hoja na dalili kwa watu wenye imani ya yakini juu ya Mwenyezi Mungu na Sheria Yake.
Na katika kupishana usiku na mchana na kufuatana katika kuwajilia na mvua Aliyoiteremsha Mwenyezi Mungu kutoka mawinguni, Akaihuisha kwayo ardhi baada ukavu wake, ikajitikisa kwa mimea na mazao, na katika kuupeleka upepo kwenu kutoka sehemu zote na kuusarifu kwa maslahi yenu, kuna dalili na hoja kwa watu wanaoelewa kuhusu Mwenyezi Mungu hoja Zake na dalili Zake.
Aya hizi na hoja tunakusomea wewe, ewe Mtume, kwa haki. Basi ni mazungumzo gani baada ya Mwenyezi Mungu na dalili Zake kuwa Yeye Ndiye Mola wa kweli Peke Yake, Hana mshirika Wake, wao watayaamini na kuyasadiki na kuyatumia?
Maangamivu makubwa yatampata kila mrongo sana mwenye dhambi nyingi.
Anayezisikia aya za kitabu cha Mwenyezi Mungu akisomewa kisha akaendelea kwenye ukanushaji wake kwa kujiona ni mkubwa zaidi wa kutoweza kumfuata Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kama kwamba yeye hakusikia alichosomewa miongoni mwa aya za Mwenyezi Mungu. Basi mbashirie, ewe Mtume, huyo mrongo sana mwenye dhambi nyingi adhabu yenye uchungu inayoumiza ndani ya Moto wa Jahanamu Siku ya Kiyama.
Na huyu mrongo sana mwingi wa dhambi anapojua kitu katika aya zetu anazifanyia shere na mzaha. Hao watakuwa na adhabu itakayowadhakikisha na kuwatia kwenye hizaya Siku ya Kiyama, ikiwa ni malipo ya kuicheza shere kwao Qur’ani.
Basi mbele ya hao wenye kuzifanyia shere aya za Mwenyezi Mungu patakuwa na moto wa Jahanamu. Na hakitawafalia wao kitu chochote kile walichokichuma cha mali na wana wala waungu wao waliowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Na watakuwa na adhabu kubwa yenye uchungu.
Hii Qur’ani tuliyoiteremsha kwako, ewe Mtume, ni uongofu wenye kuondoa upotevu, ni dalili ya haki na inamuongoza kwenye njia iliyolingana sawa atakayeifuata na akaifanyia kazi. Na wale waliozikataa aya zilizomo ndani ya Qur’ani zenye kutolea dalili Ukweli na wasiziamini, watakuwa na adhabu miongoni mwa adhabu kali zaidi Siku ya Kiyama, yenye uchungu na kuumiza.
Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, Ndiye Aliyewadhalilishia bahari, ili majahazi yatembee juu yake kwa amri Yake, na ili mtafute kheri Zake kwa biashara mbalimbali na shughuli za kuchuma, na kwamba nyinyi mpate kumshukuru Mola wenu kuwadhalilishia hayo, na hivyo basi mumuabudu Yeye Peke Yake na mumtii Yeye katika yale Anayowaamrisha na kuwakataza.
Na Akawadhalilishia kila kilichoko mbinguni miongoni mwa jua , mwezi na nyota, na kila kilicho ardhini miongoni mwa wanyama, miti, majahazi na visiokuwa hivyo kwa ajili ya maslahi yenu. Neema zote hizi ni vipaji Alizowaneemesha nazo Mwenyezi Mungu Peke Yake na fadhila inayotoka Kwake Aliyowafadhili nayo. Basi Yeye Peke Yake muabuduni, na msimfanye yoyote kuwa ni mshirika Wake. Hakika katika vitu vile Alivyowadhalilishia Mwenyezi Mungu kuna alama na dalili juu ya upweke wa Mwenyezi Mungu kwa watu wenye kuzitia akilini aya za Mwenyezi Mungu, hoja Zake na dalili Zake, wakazizingatia.
Sema, ewe Mtume, uwaambie wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na wakamfuata Mtume Wake, wawasamehe na kuwaachilia wale ambao hawana matarajio ya malipo mema ya Mwenyezi Mungu na hawaogopi adhabu Yake wanapowakusudia Waumini kuwaudhi na kuwakera, ili Mwenyezi Mungu Awalipe washirikina hawa kwa yale waliyoyachuma duniani ya madhambi na kuwaudhi Waumini.
Yoyote yule, miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu, Anayefanya matendo ya utiifu Kwake, basi malipo mema ya utiifu wake atayapata mwenyewe, na mwenye kufanya matendo mabaya duniani kwa kumuasi Mwenyezi Mungu, basi atakuwa amejikosea mwenyewe. Kisha nyinyi, enyi watu, mtaishia kwa Mola wenu baada ya kufa kwenu, Amlipe mwema kwa wema wake na mbaya kwa ubaya wake.
Hakika tuliwapatia Wana wa Isrāīl Taurati na Injili na tukawaamuru kuhukumu kulingana na yaliyomo kwenye vitabu viwili hivyo, na tukawafanya wengi wa Manabii watokanao na kizazi cha Ibrāhīm, amani imshukie, ni katika wao, na tukawaruzuku vitu vizuri miongoni mwa vitu vya kukimu maisha, matunda na vyakula, na tukawafadhilisha juu ya walimwengu wa zama zao.
Na tukawapatia Wana wa Isrāīl Sheria zilizo wazi juu ya halali na haramu, na dalili zenye kutenganisha haki na batili. Hawakutafautiana isipokuwa baada ya kujiwa na elimu na hoja ikasimama juu yao. Na lililowapelekea wafanye hivyo ni lile jambo la kudhulumiana wao kwa wao kwa kutaka ukubwa na uongozi. Hakika Mola wako Atahukumu baina ya wanaotafautiana miongoni mwa Wana wa Isrāīl Siku ya Kiyama katika yale waliokuwa wakitafautiana juu yake duniani. Kwenye maelezo haya pana onyo kwa ummah huu wasifuate mwenendo wao.
Kisha tukakufanya, ewe Mtume, uwe kwenye njia iliyofunuka wazi kuhusu jambo la Dini. Basi fuata Sheria ambayo Mwenyezi Mungu Amekupatia, na usifuate matamanio ya wajinga wa Sheria ya Mwenyezi Mungu, wasiojua haki. Katika hii aya kuna ushahidi mkubwa juu ya ukamilifu wa Dini hii na utukufu wake na ulazima wa kufuata hukumu zake na kutopotoka kuelemea kwenye matamanio ya makafiri na wapotofu.
Hawa waliomshirikisha Mola wao wanaokuita ufuate matamanio yao, hawatakufalia kitu, ewe Mtume, kwa kukuepushia adhabu ya Mwenyezi Mungu iwapo umefuata matamanio yao. Na hakika madhalimu wenye kukiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu miongoni mwa wanafiki, Mayahudi na wasiokuwa hao wanasaidiana wao kwa wao dhidi ya wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na walio watiifu Kwake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwapa ushindi wenye kumcha Mola wao kwa kutekeleza faradhi Zake na kujiepusha na makatazo Yake.
Hii Qur’ani tuliyokuteremshia, ewe Mtume, ni miangaza ya watu kuiona haki na kuipambanua na batili, na kuijua kwayo njia ya usawa, na ni uongofu na rehema kwa watu wenye kuwa na Imani ya yakini juu ya uhakika wa usahihi wake, na kwamba hiyo ni teremsho kutoka kwa Mshindi Mwenye hekima.
Bali je, wanadhani wale wanaotenda maovu na wanaowakanusha Mitume wa Mwenyezi Mungu na kuenda kinyume na amri ya Mola wao na wakamuabudu asiyekuwa Yeye, kuwa tutawafanya wao ni kama wale wanaomuamini Mwenyezi Mungu na wakawasadiki Mitume Wake na wakafanya matendo mema na wakamtakasia Yeye ibada na sio wengine, na tuwasawazishe na wao ulimwenguni na Akhera? Ni uamuzi mbaya huo wao wa kuwsawazisha baina ya waovu na wema kesho Akhera.
Na Mwenyezi Mungu Ameumba mbingu na ardhi kwa haki, uadilifu na hekima , na ili kila nafsi ilipwe huko Akhera kwa ilichokitenda cha kheri au cha shari, na wao hawatadhulumiwa malipo ya matendo yao.
Unamuona vipi, ewe Mtume, yule aliyoyachukuwa matamanio yake akayafanya ndiye Mola wake, akawa hatamani kitu isipokuwa anakifanya, na Mwenyezi Mungu Akampoteza baada ya ujuzi kumfikia na kusimamiwa na hoja, akawa hasikii mawaidha ya Mwenyezi Mungu wala hazingatii kwa mawaidha hayo, na Mwenyezi Mungu akapiga muhuri juu ya moyo wake akawa hafahamu kitu, na Akaweka finiko kwenye macho yake akawa hazioni hoja za Mwenyezi Mungu? Basi ni nani atakayemuongoza kuifikia haki na uongofu baada ya Mwenyezi Mungu kumpoteza? Kwani hamkumbuki, enyi watu mkajua kwamba mwenye kufanywa hivyo na Mwenyezi Mungu hataongoka kabisa na hatapata wa kumsaidia na kumuongoza? Aya hii ndio msingi wa kuonya kwamba matamanio hayafai kuwa ndio msukumo wa Waumini katika matendo yao.
Na wanasema hawa washirikina, “Hakuna maisha isipokuwa haya maisha yetu ya duniani tuliyonayo; hakuna maisha mengineyo,” kwa njia ya kukanusha kufufuliwa baada ya kufa. “Na hakuna kinachotuangamiza isipokuwa kupitiwa na masiku na michana na umri mrefu,“ wakikanusha kuwa wana Mola Anaowatowesha na kuwaangamiza.” Na hawa washirikina hawana ujuzi wowote juu ya hilo, hawana lolote isipokuwa ni kusema kwa kudhania, kufikiria na kuwaza.
Na wanaposomewa, hawa washirikina wakanushaji, aya zetu zilizo waziwazi, huwa hawana hoja isipokuwa ni kutoa maneno yao kumwambia Mtume Muhammad, “Wahuishe, wewe na Waumini, baba zetu waliokufa iwapo nyinyi ni wakweli kwa mnayoyasema.”
Sema, ewe Mtume, uwaambie hawa washirikina wenye kukanusha kufufuliwa, “Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, Atawahuisha duniani kipindi Anachotaka muishi, kisha Atawafisha humo, kisha Atawakusanya mkiwa hai kwenye Siku ya Kiyama isiyokuwa na shaka.» Lakini wengi wa watu hawajui kwamba Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwafisha, kisha kuwafufua Siku ya Kiyama.
Ni ya Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika, mamlaka ya mbingu saba na ardhi kwa kuziumba, kuzimiliki na kuwa ziko chini ya amri Yake. Na siku Kiyama kitakapokuja ambapo wafu watafufuliwa kutoka kwenye makaburi yao na watahesabiwa, hapo watapata hasara wale waliomkanusha Mwenyezi Mungu na kukataa kile Alichomteremshia Mtume Wake miongoni mwa aya zilizbainika na dalili zilizofunuka wazi.
Utaona, ewe Mtume, Siku ya Kiyama, watu wa kila mila na dini wamepiga magoti, kila ummah wanaitwa kushuhudia kitabu matendo yao, na wataambiwa, «Leo mtalipwa kwa yale mliokuwa mkiyafanya ya kheri au ya shari.
«Hiki ni Kitabu chetu kinatamka kuhusu matendo yenu yote, bila kuongeza wala kupunguza. Sisi tulikuwa tukiwaamrisha Watunzi wenye kudhibiti wayaandike matendo yenu.»
Ama wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake duniani, wakafuata amri Zake na wakajiepusha makatazo Yake, hao Atawatia Mola wao kwenye Pepo Yake kwa rehema Zake. Kuingia huko ndiko kufaulu kuliko wazi ambako hakuna kufaulu kupita huko.
Na ama wale waliokataa kuwa Mwenyezi Mungu Ndiye Mola wa haki, wakawakanusha Mitume Wake, na wasifuate Sheria Yake kivitendo, basi wataambiwa kwa kukaripiwa na kulaumiwa, «Kwani aya zangu hazikuwa zikisomwa kwenu huko duniani, mkazifanyia kiburi kwa kutozisikiliza na kutoziamini, na mkawa ni watu wenye kushirikisha, mnachuma maasia na hamuamini thawabu wala mateso?»
Na mnapoambiwa, «Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ya kuwafufua watu kutoka kwenye makaburi yao ni kweli, na kwamba kipindi cha kusimama Kiyama ni jambo lisilo na shaka, mnasema, ‘Hatujui ni nini Kiyama? Na hatudhani kuwa kitatokea isipokuwa ni kudhania tu, na sisi si wenye uhakika kuwa kipindi hicho cha Kiyama ni chenye kuja.’»
Na yakawafunukia hawa waliokuwa wakizikanusha aya za Mwenyezi Mungu yale matendo mabaya waliyoyafanya ulimwenguni, na ikawateremkia adhabu ya Mwenyezi Mungu ikiwa ni malipo ya yale waliokuwa wakiyafanyia shere.
Na wakaambiwa hao makafiri, «Leo tutawaacha ndani ya adhabu ya Moto wa Jahanamu, kama vile mlivyoacha kumuamini Mola wenu na kufanya matendo ya kuwafaa katika makutano ya Siku yenu hii, na makao yenu ni Moto wa Jahanamu, na hamtakuwa na wasaidizi wenye kuwaokoa na adhabu ya Mwenyezi Mungu.
«Haya yaliyowafika ya adhabu ya Mwenyezi Mungu ni kwa sababu ya kuwa nyinyi mlizifanya aya za Mwenyezi Mungu na hoja Zake kuwa shere na mchezo, na likawadanganya nyinyi pambo la uhai wa kilimwengu.» Basi Leo hawatatolewa Motoni wala hawatarudishwa ulimwenguni ili watubie na wafanye mema.
Basi ni za Mwenyezi Mungu, kutakasika ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Peke Yake, shukrani zote kwa neema Zake zisizohesabika kwa viumbe Vyake, Mola wa mbingu na ardhi na Mwenye kuziumba na kuziendesha, Mola wa viumbe Wote.
Na ni wake Peke Yake utukufu, haiba, enzi, utawala, uweza na ukamilifu, mbinguni na ardhini. Na Yeye Ndiye Mshindi Asiyekuwa na mshindani mwenye kushindana na Yeye, Mwingi wa hekima katika maneno Yake, vitendo Vyake, upangaji Wake na Sheria Zake, Ametukuka na kutakasika, hapana Mola isipokuwa Yeye.