Sura Qaf kwa Kiswahili

Kaaf · سورة ق

Makka Aya: 45 Juzuu 26 Ukurasa 518 Mpangilio wa kuteremshwa: 34

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

قٓۚ وَٱلۡقُرۡءَانِ ٱلۡمَجِيدِ ١

«Qāf» Yametangulia maelezo kuhusu herufi zilizokatwa na kutengwa mwanzoni mwa sura ya Al-Baqarah. Anaapa Mwenyezi Mungu kwa Qur’ani tukufu, yenye ubora na heshima.

بَلۡ عَجِبُوٓاْ أَن جَآءَهُم مُّنذِرࣱ مِّنۡهُمۡ فَقَالَ ٱلۡكَٰفِرُونَ هَٰذَا شَيۡءٌ عَجِيبٌ ٢

Bali wale wenye kumkanusha Mtume waliona ajabu kuwa walijiwa na muonyaji miongoni mwao anayewaonya mateso ya Mwenyezi Mungu, basi wale waliomkufuru Mwenyezi Mungu na Mtume Wake walisema, «Hili ni jambo geni la kuonewa ajabu.

أَءِذَا مِتۡنَا وَكُنَّا تُرَابࣰاۖ ذَٰلِكَ رَجۡعُۢ بَعِيدࣱ ٣

«Je, tunapokufa na tukawa mchanga, itawezekana vipi kurejea baada ya hapo tukawa kama tulivyokuwa? Hayo ni marajeo ambayo kutukia kwake kuko mbali.»

قَدۡ عَلِمۡنَا مَا تَنقُصُ ٱلۡأَرۡضُ مِنۡهُمۡۖ وَعِندَنَا كِتَٰبٌ حَفِيظُۢ ٤

Hakika tunakijua kile ambacho ardhi kinakipunguza na kukimaliza katika miili yao, na tuna Kitabu kilichohifadhiwa kutokana na mageuzo na mabadiliko, kilichosajiliwa kila kitu kitakachowapitia katika maisha yao na baada ya kufa kwao.

بَلۡ كَذَّبُواْ بِٱلۡحَقِّ لَمَّا جَآءَهُمۡ فَهُمۡ فِيٓ أَمۡرࣲ مَّرِيجٍ ٥

Bali hawa washirikina waliikanusha Qur’ani ilipowajia. Wao wako kwenye hali ya babaiko na kuchanganyikiwa, hawasimami imara kwenye jambo lolote, na hawana kituo cha kutulia.

أَفَلَمۡ يَنظُرُوٓاْ إِلَى ٱلسَّمَآءِ فَوۡقَهُمۡ كَيۡفَ بَنَيۡنَٰهَا وَزَيَّنَّٰهَا وَمَا لَهَا مِن فُرُوجࣲ ٦

Kwani walighafilika walipokanusha Ufufuzi, wasianagalie mbingu juu yao: vipi tulizijenga zikiwa zimelingana sawa pande zote, limeimarika jengo lake, na tukazipamba kwa nyota, na hazina pasuko na nyufa, zimesalimika na hitilafu na kasoro?

وَٱلۡأَرۡضَ مَدَدۡنَٰهَا وَأَلۡقَيۡنَا فِيهَا رَوَٰسِيَ وَأَنۢبَتۡنَا فِيهَا مِن كُلِّ زَوۡجِۭ بَهِيجࣲ ٧

Na ardhi tumeipanua na kuitandika, na tukaweka humo majabali yaliyojikita, ili ardhi isiende mrama na watu wake, na tukaotesha humo kila aina ya mimea yenye mandhari ya kupendeza na yenye kunufaisha, inayomfurahisha mwenye kuiangalia.

تَبۡصِرَةࣰ وَذِكۡرَىٰ لِكُلِّ عَبۡدࣲ مُّنِيبࣲ ٨

Mwenyezi Mungu Ameumba mbingu, ardhi na vilivyomo baina ya hivyo viwili miongoni mwa alama kubwa, ili viwe ni mazingatio ya kumfanya mtu aone na atoke kwenye giza la ujinga, na ni ukumbusho kwa kila mja mnyenyekevu, mwenye kucha na kuogopa, mwenye kurejea sana kwa Mwenyezi Mungu Aliyeshinda na kutukuka.

وَنَزَّلۡنَا مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءࣰ مُّبَٰرَكࣰا فَأَنۢبَتۡنَا بِهِۦ جَنَّٰتࣲ وَحَبَّ ٱلۡحَصِيدِ ٩

Na tumeteremsha kutoka juu mvua yenye manufaa mengi, tukaotesha kwayo mabustani yenye miti mingi na nafaka za mimea ya nafaka zinazovunwa.

وَٱلنَّخۡلَ بَاسِقَٰتࣲ لَّهَا طَلۡعࣱ نَّضِيدࣱ ١٠

Na tukaotesha mitende mirefu yenye makarara yaliyojaza na kupandana.

رِّزۡقࣰا لِّلۡعِبَادِۖ وَأَحۡيَيۡنَا بِهِۦ بَلۡدَةࣰ مَّيۡتࣰاۚ كَذَٰلِكَ ٱلۡخُرُوجُ ١١

Tumeviotesha hivyo viwe ni riziki za waja za wao kuzila kulingana na mahitaji yao, na tukahuisha, kwa maji haya tuliyoyateremsha, ardhi iliyokuwa kavu na kame, haina nafaka wala mimea mingine. Na kama tunavyohuisha, kwa maji hayo, ardhi iliyokufa, tutawatoa nyinyi Siku ya Kiyama mkiwa hai baada ya kufa.

كَذَّبَتۡ قَبۡلَهُمۡ قَوۡمُ نُوحࣲ وَأَصۡحَٰبُ ٱلرَّسِّ وَثَمُودُ ١٢

Walikanusha, kabla ya hawa washirikina miongoni mwa Makureshi, watu wa Nūḥ, watu wa Kisima na Thamūd.

وَعَادࣱ وَفِرۡعَوۡنُ وَإِخۡوَٰنُ لُوطࣲ ١٣

Na 'Ād na Fir'awn na watu wa Lūṭ.

وَأَصۡحَٰبُ ٱلۡأَيۡكَةِ وَقَوۡمُ تُبَّعࣲۚ كُلࣱّ كَذَّبَ ٱلرُّسُلَ فَحَقَّ وَعِيدِ ١٤

Na watu waliokuwa kwenye tuka la miti nao ni watu wa Shu'ayb, na watu wa Tubba' wa Himyar. Watu wote hao waliwakanusha Mitume wao, ikapasa juu yao adhabu ambayo Mwenyezi Mungu Aliwaonya nayo kwa ukafiri wao.

أَفَعَيِينَا بِٱلۡخَلۡقِ ٱلۡأَوَّلِۚ بَلۡ هُمۡ فِي لَبۡسࣲ مِّنۡ خَلۡقࣲ جَدِيدࣲ ١٥

Kwani tulishindwa kuanzisha uumbaji wa kwanza tuliyouanzisha na hakukuwa na kitu chochote, mpaka tushindwe kuwarudisha wao wakiwa viumbe wapya baada ya kutoweka kwao? Hilo halitushindi. Bali sisi ni waweza wa hilo, lakini wao wako kwenye mshangao na shaka juu ya jambo la kufufuliwa na kukusanywa.

وَلَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ وَنَعۡلَمُ مَا تُوَسۡوِسُ بِهِۦ نَفۡسُهُۥۖ وَنَحۡنُ أَقۡرَبُ إِلَيۡهِ مِنۡ حَبۡلِ ٱلۡوَرِيدِ ١٦

Hakika tumemuumba binadamu na tunakijua kile ambacho nafsi yake inamhadithia kwacho. Na sisi tuko karibu na yeye zaidi kuliko ukambaa wa roho (nao ni mshipa ulioko shingoni unaoshikana na moyo).

إِذۡ يَتَلَقَّى ٱلۡمُتَلَقِّيَانِ عَنِ ٱلۡيَمِينِ وَعَنِ ٱلشِّمَالِ قَعِيدࣱ ١٧

Pindi Malaika wawili wanaotunza, kuliani kwake na kushotoni kwake, wanapoyaandika matendo Yake: aliye kuliani anaandika mema na aliye kushotoni anaandika maovu.

مَّا يَلۡفِظُ مِن قَوۡلٍ إِلَّا لَدَيۡهِ رَقِيبٌ عَتِيدࣱ ١٨

Hatamki neno kulisema isipokuwa mbele yake pana Malaika anayetunza maneno yake na kuyaandika, naye ni Malaika ambaye yupo wakati wote aliyeandaliwa kwa hilo.

وَجَآءَتۡ سَكۡرَةُ ٱلۡمَوۡتِ بِٱلۡحَقِّۖ ذَٰلِكَ مَا كُنتَ مِنۡهُ تَحِيدُ ١٩

Na hapo ikaja shida ya mauti na kizaazaa chake na ukweli usiozuilika wala kukimbilika! Hali hiyo ndiyo ambayo ulikuwa, ewe binadamu, ukiikimbia na kuihepa.

وَنُفِخَ فِي ٱلصُّورِۚ ذَٰلِكَ يَوۡمُ ٱلۡوَعِيدِ ٢٠

Hapo baragumu likavuviwa mvuvio wa pili wa Ufufuzi. Mvuvio huo utakuwa kwenye Siku ya matekelezo ya adhabu ambayo Mwenyezi Mungu Aliwaahidi wakanushaji.

وَجَآءَتۡ كُلُّ نَفۡسࣲ مَّعَهَا سَآئِقࣱ وَشَهِيدࣱ ٢١

Na ije kila nafsi, wakiwa pamoja nayo Malaika wawili: mmoja anaiongoza kwenye Mkusanyiko, na mwingine Anaitolea ushahidi wa ililolifanya duniani, la kheri na shari.

لَّقَدۡ كُنتَ فِي غَفۡلَةࣲ مِّنۡ هَٰذَا فَكَشَفۡنَا عَنكَ غِطَآءَكَ فَبَصَرُكَ ٱلۡيَوۡمَ حَدِيدࣱ ٢٢

Kwa hakika wewe ulikuwa katika mghafala kuhusu tukio hili unaloliona leo, ewe binadamu, ndipo tukakifunua kifiniko chako kilichoziba moyo wako, kughafilika kukakuondokea, basi leo macho yako, katika kile unachokitolea ushahidi, ni makali.

وَقَالَ قَرِينُهُۥ هَٰذَا مَا لَدَيَّ عَتِيدٌ ٢٣

Na Malaika mwandishi mwenye kumtolea ushahidi atasema, «Haya ndiyo niliyonayo kutoka kwenye rikodi ya matendo yake. Nayo imetayarishwa, imehifadhiwa na ipo hapa kwangu.»

أَلۡقِيَا فِي جَهَنَّمَ كُلَّ كَفَّارٍ عَنِيدࣲ ٢٤

Na Mwenyezi Mungu Aseme kuwaambia Malaika wawili: mwenye kuongoza na yule shahidi, baada ya kutolewa uamuzi baina ya viumbe, «Mtupeni ndani ya Jahanamu kila mwenye kukataa kuwa Mwenyezi Mungu Ndiye Mola wa haki, aliye mwingi wa ukafiri na ukanushaji, mwenye kuipinga haki,

مَّنَّاعࣲ لِّلۡخَيۡرِ مُعۡتَدࣲ مُّرِيبٍ ٢٥

mwenye kuzuia kutekeleza haki zilizo juu yake katika mali yake, anaye wadhulumu waja wa Mwenyezi Mungu na kukiuka mipaka Yake, anayelifanyia shaka agizo la Mwenyezi Mungu na onyo Lake,

ٱلَّذِي جَعَلَ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَ فَأَلۡقِيَاهُ فِي ٱلۡعَذَابِ ٱلشَّدِيدِ ٢٦

aliyemshirikisha Mwenyezi Mungu kwa kukiabudu kiabudiwa kingine miongoni mwa viumbe Vyake pamoja na Yeye. Mtupeni ndani ya adhabu ya moto wa Jahanamu ulio mkali.»

۞ قَالَ قَرِينُهُۥ رَبَّنَا مَآ أَطۡغَيۡتُهُۥ وَلَٰكِن كَانَ فِي ضَلَٰلِۭ بَعِيدࣲ ٢٧

Shetani wake aliyekuwa na yeye ulimwenguni atasema, «Mola wetu! Mimi sikumpoteza, lakini alikuwa kwenye njia iliyokuwa mbali na njia ya uongofu.»

قَالَ لَا تَخۡتَصِمُواْ لَدَيَّ وَقَدۡ قَدَّمۡتُ إِلَيۡكُم بِٱلۡوَعِيدِ ٢٨

Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Aseme, «Msitete mbele yangu leo kwenye Kisimamo cha Malipo na Hesabu. Kwani hilo halina faida, na mimi niliwaletea duniani onyo la adhabu kwa aliyenikufuru na kuniasi.

مَا يُبَدَّلُ ٱلۡقَوۡلُ لَدَيَّ وَمَآ أَنَا۠ بِظَلَّٰمࣲ لِّلۡعَبِيدِ ٢٩

«Halibadilishwi neno kwangu, na simuadhibu yoyote kwa dhambi za mtu mwingine, simuadhibu yoyote isipokuwa kwa dhambi zake baada ya kusimamiwa na hoja.»

يَوۡمَ نَقُولُ لِجَهَنَّمَ هَلِ ٱمۡتَلَأۡتِ وَتَقُولُ هَلۡ مِن مَّزِيدࣲ ٣٠

Watajie watu wako, ewe Mtume, Siku tutakayoiambia Jahanamu, «Je umeshajaa?» Na Jahanamu iseme, «Je kuna nyongeza yoyote ya majini na binadamu?» Hapo Mola, uliotukuka utukufu wake, Aweke unyayo Wake ndani yake, na hapo ijikusanye na ijikunjekunje na iseme, «Basi! Basi!»

وَأُزۡلِفَتِ ٱلۡجَنَّةُ لِلۡمُتَّقِينَ غَيۡرَ بَعِيدٍ ٣١

Na hapo wachamungu wakaribishiwe Pepo, iwepo mahali ambapo si mbali na wao, wawe waiona, kwa kuwaongezea furaha zao.

هَٰذَا مَا تُوعَدُونَ لِكُلِّ أَوَّابٍ حَفِيظࣲ ٣٢

Na waambiwe hao Waumini, «Hii ndiyo ile mliokuwa mkiahidiwa, enyi wachamungu, kwa kila mtubiaji dhambi zake, mwenye kukitunza kila kinachomkurubisha kwa Mola Wake miongoni mwa mambo ya lazima na ya utiifu;

مَّنۡ خَشِيَ ٱلرَّحۡمَٰنَ بِٱلۡغَيۡبِ وَجَآءَ بِقَلۡبࣲ مُّنِيبٍ ٣٣

mwenye kumcha Mwenyezi Mungu duniani na akakutana na Yeye Siku ya Kiyama kwa moyo wa mwenye kutubia dhambi zake.»

ٱدۡخُلُوهَا بِسَلَٰمࣲۖ ذَٰلِكَ يَوۡمُ ٱلۡخُلُودِ ٣٤

Na hapo waambiwe hao Waumini, «Ingieni Peponi kuingia kunakoshikamana na kusalimika na maafa na shari, hali ya kuhifadhiwa na mambo yote mnayoyachukia. Hiyo ndiyo Siku ya starehe za milele zisizokatika.»

لَهُم مَّا يَشَآءُونَ فِيهَا وَلَدَيۡنَا مَزِيدࣱ ٣٥

Watapewa hawa Waumini ndani ya Pepo wanavyovitaka. Na tuna nyogeza za neema juu ya zile tulizowapa; kubwa zaidi la neema hizo ni kutazama uso wa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka.

وَكَمۡ أَهۡلَكۡنَا قَبۡلَهُم مِّن قَرۡنٍ هُمۡ أَشَدُّ مِنۡهُم بَطۡشࣰا فَنَقَّبُواْ فِي ٱلۡبِلَٰدِ هَلۡ مِن مَّحِيصٍ ٣٦

Na tuliwaangamiza, kabla ya hao washirikina wa Kikureshi, ummah wengi. Walikuwa wana nguvu na ujebari kuliko wao. Walizunguka mijini wakafuata kila njia kutaka kuyakimbia maangamivu. Basi je, kuna makimbilizi yoyote ya kujiepusha na adhabu ya Mwenyezi Mungu itakapowajia?

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَذِكۡرَىٰ لِمَن كَانَ لَهُۥ قَلۡبٌ أَوۡ أَلۡقَى ٱلسَّمۡعَ وَهُوَ شَهِيدࣱ ٣٧

Hakika katika kuziangamiza kame zilizopita kuna mazingatio kwa aliyekuwa na moyo wa kufahamia na mashikio ya kusikilizia, na akawa yupo kwa moyo wake, hakusahau wala hakughafilika

وَلَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَمَا بَيۡنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامࣲ وَمَا مَسَّنَا مِن لُّغُوبࣲ ٣٨

Na kwa hakika tuliumba mbingu na ardhi na vilivyoko baina ya hivyo viwili miongoni mwa viumbe kwa muda wa Siku sita, na hatukupata tabu yoyote wala shida. Katika uweza huu mkubwa kuna dalili ya nguvu zaidi ya kuwa Yeye, Aliyetakasika, Ana uweza wa kuhuisha wafu.

فَٱصۡبِرۡ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَسَبِّحۡ بِحَمۡدِ رَبِّكَ قَبۡلَ طُلُوعِ ٱلشَّمۡسِ وَقَبۡلَ ٱلۡغُرُوبِ ٣٩

Basi vumilia, ewe Mtume, kwa yale wanayoyasema wakanushaji, kwani Mwenyezi Mungu Yuko chonjo nao. Na swali, kwa ajili ya Mola wako kwa kumshukuru, Swala ya Alfajiri, kabla ya jua kuchomoza, na Swala ya Alasiri kabla ya jua kuchwa,

وَمِنَ ٱلَّيۡلِ فَسَبِّحۡهُ وَأَدۡبَٰرَ ٱلسُّجُودِ ٤٠

na uswali kipindi cha usiku na umtakase Mola Wako kwa kumshukuru baada ya Swala.

وَٱسۡتَمِعۡ يَوۡمَ يُنَادِ ٱلۡمُنَادِ مِن مَّكَانࣲ قَرِيبࣲ ٤١

Na usikilize, ewe Mtume, siku Malaika atakapoita kwa kupuliza kwenye Baragumu kutoka sehemu iliyo karibu.

يَوۡمَ يَسۡمَعُونَ ٱلصَّيۡحَةَ بِٱلۡحَقِّۚ ذَٰلِكَ يَوۡمُ ٱلۡخُرُوجِ ٤٢

Siku watakapousikia ukulele wa Ufufuzi wa ukweli usio na shaka, hiyo ndiyo Siku ya waliyo makaburini kutoka makaburini mwao.

إِنَّا نَحۡنُ نُحۡيِۦ وَنُمِيتُ وَإِلَيۡنَا ٱلۡمَصِيرُ ٤٣

Ni sisi tunaohuisha viumbe na kuwafisha duniani, na ni kwetu sisi ndipo mwisho wao wote watakapofikia Siku ya Kiyama ili wahesabiwe na walipwe.

يَوۡمَ تَشَقَّقُ ٱلۡأَرۡضُ عَنۡهُمۡ سِرَاعࣰاۚ ذَٰلِكَ حَشۡرٌ عَلَيۡنَا يَسِيرࣱ ٤٤

Siku ambayo ardhi itapasukapasuka itoe wafu waliozikwa humo, watoke mbio kuelekea upande wa yule anayeita. Kuwakusanya watu hivyo kwenye Kisimamo cha Hesabu ni jambo sahali kwetu na rahisi.

نَّحۡنُ أَعۡلَمُ بِمَا يَقُولُونَۖ وَمَآ أَنتَ عَلَيۡهِم بِجَبَّارࣲۖ فَذَكِّرۡ بِٱلۡقُرۡءَانِ مَن يَخَافُ وَعِيدِ ٤٥

Sisi ni wajuzi zaidi kwa wanayoyasema hawa washirikina, ya kumzulia Mwenyezi Mungu urongo na kukanusha aya Zake. Na hukuwa wewe, ewe Mtume, umepewa nguvu juu yao ya kuwalazimisha waingie katika Uislamu, hakika ni kwamba wewe umetumilizwa uwe mfikishaji. Basi mkumbushe kwa Qur’ani anayeogopa onyo langu, kwa kuwa asiyeogopa onyo (la Mwenyezi Mungu) hafaidiki kwa kukumbushwa.

Tafsiri nyingine za sura hii

Tafsiri ya sura hii kwa Kiarabu Abdullah Muhammad & Nassir Khamis

Sura

1 Al-Fatihah Al-Fatiha · aya 7 · Makka Juzuu 1 · Iliteremshwa ya 5 الفاتحة 2 Al-Baqarah Al-Bakarah · aya 286 · Madina Juzuu 1 · Iliteremshwa ya 87 البقرة 3 Al-Imran Al-Imaran · aya 200 · Madina Juzuu 3 · Iliteremshwa ya 89 آل عمران 4 An-Nisa' An-Nisa'i · aya 176 · Madina Juzuu 4 · Iliteremshwa ya 92 النساء 5 Al-Ma'idah aya 120 · Madina Juzuu 6 · Iliteremshwa ya 112 المائدة 6 Al-An'am aya 165 · Makka Juzuu 7 · Iliteremshwa ya 55 الأنعام 7 Al-A'raf Al-A'araf · aya 206 · Makka Juzuu 8 · Iliteremshwa ya 39 الأعراف 8 Al-Anfal Al'Anfal · aya 75 · Madina Juzuu 9 · Iliteremshwa ya 88 الأنفال 9 At-Taubah aya 129 · Madina Juzuu 10 · Iliteremshwa ya 113 التوبة 10 Yunus aya 109 · Makka Juzuu 11 · Iliteremshwa ya 51 يونس 11 Hood Hud · aya 123 · Makka Juzuu 11 · Iliteremshwa ya 52 هود 12 Yusuf aya 111 · Makka Juzuu 12 · Iliteremshwa ya 53 يوسف 13 Ar-Ra'd Ra'ad · aya 43 · Madina Juzuu 13 · Iliteremshwa ya 96 الرعد 14 Ibrahim aya 52 · Makka Juzuu 13 · Iliteremshwa ya 72 إبراهيم 15 Al-Hijr A-Hijr · aya 99 · Makka Juzuu 14 · Iliteremshwa ya 54 الحجر 16 An-Nahl aya 128 · Makka Juzuu 14 · Iliteremshwa ya 70 النحل 17 Al-Isra Al-Isra'i · aya 111 · Makka Juzuu 15 · Iliteremshwa ya 50 الإسراء 18 Al-Kahf aya 110 · Makka Juzuu 15 · Iliteremshwa ya 69 الكهف 19 Maryam Marya · aya 98 · Makka Juzuu 16 · Iliteremshwa ya 44 مريم 20 Ta­Ha Taha · aya 135 · Makka Juzuu 16 · Iliteremshwa ya 45 طه 21 Al-Anbiya' Al-Anbiya · aya 112 · Makka Juzuu 17 · Iliteremshwa ya 73 الأنبياء 22 Al-Hajj aya 78 · Madina Juzuu 17 · Iliteremshwa ya 103 الحج 23 Al-Mu'minun Al-Muminu · aya 118 · Makka Juzuu 18 · Iliteremshwa ya 74 المؤمنون 24 An-Nur aya 64 · Madina Juzuu 18 · Iliteremshwa ya 102 النور 25 Al-Furqan Al-Furkan · aya 77 · Makka Juzuu 18 · Iliteremshwa ya 42 الفرقان 26 Ash-Shu'ara' As-Shu'ara · aya 227 · Makka Juzuu 19 · Iliteremshwa ya 47 الشعراء 27 An-Naml aya 93 · Makka Juzuu 19 · Iliteremshwa ya 48 النمل 28 Al-Qasas Al-Kasas · aya 88 · Makka Juzuu 20 · Iliteremshwa ya 49 القصص 29 Al-'Ankabut Al-Ankabut · aya 69 · Makka Juzuu 20 · Iliteremshwa ya 85 العنكبوت 30 Ar­Room Ar-Rum · aya 60 · Makka Juzuu 21 · Iliteremshwa ya 84 الروم 31 Luqman Lukuman · aya 34 · Makka Juzuu 21 · Iliteremshwa ya 57 لقمان 32 As­Sajdah As-Sajadah · aya 30 · Makka Juzuu 21 · Iliteremshwa ya 75 السجدة 33 Al­Ahzab Al-Ahzab · aya 73 · Madina Juzuu 21 · Iliteremshwa ya 90 الأحزاب 34 Saba' Saba'i · aya 54 · Makka Juzuu 22 · Iliteremshwa ya 58 سبأ 35 Fatir aya 45 · Makka Juzuu 22 · Iliteremshwa ya 43 فاطر 36 Ya­Sin Yasin · aya 83 · Makka Juzuu 22 · Iliteremshwa ya 41 يس 37 As-Saffat aya 182 · Makka Juzuu 23 · Iliteremshwa ya 56 الصافات 38 Sad aya 88 · Makka Juzuu 23 · Iliteremshwa ya 38 ص 39 Az-Zumar aya 75 · Makka Juzuu 23 · Iliteremshwa ya 59 الزمر 40 Ghafir aya 85 · Makka Juzuu 24 · Iliteremshwa ya 60 غافر 41 Fussilat aya 54 · Makka Juzuu 24 · Iliteremshwa ya 61 فصلت 42 Ash-Shura As-Shurah · aya 53 · Makka Juzuu 25 · Iliteremshwa ya 62 الشورى 43 Az-Zukhruf aya 89 · Makka Juzuu 25 · Iliteremshwa ya 63 الزخرف 44 Ad-Dukhan aya 59 · Makka Juzuu 25 · Iliteremshwa ya 64 الدخان 45 Al-Jathiya Al-Jasiyah · aya 37 · Makka Juzuu 25 · Iliteremshwa ya 65 الجاثية 46 Al-Ahqaf Al-Ahkaf · aya 35 · Makka Juzuu 26 · Iliteremshwa ya 66 الأحقاف 47 Muhammad aya 38 · Madina Juzuu 26 · Iliteremshwa ya 96 محمد 48 Al-Fath aya 29 · Madina Juzuu 26 · Iliteremshwa ya 111 الفتح 49 Al-Hujurat aya 18 · Madina Juzuu 26 · Iliteremshwa ya 106 الحجرات 50 Qaf Kaaf · aya 45 · Makka Juzuu 26 · Iliteremshwa ya 34 ق 51 Az-Zariyat aya 60 · Makka Juzuu 26 · Iliteremshwa ya 67 الذاريات 52 At-Tur aya 49 · Makka Juzuu 27 · Iliteremshwa ya 76 الطور 53 An-Najm aya 62 · Makka Juzuu 27 · Iliteremshwa ya 23 النجم 54 Al-Qamar Al-Kamar · aya 55 · Makka Juzuu 27 · Iliteremshwa ya 37 القمر 55 Ar-Rahman aya 78 · Madina Juzuu 27 · Iliteremshwa ya 97 الرحمن 56 Al-Waqi'ah Al-Waki'ah · aya 96 · Makka Juzuu 27 · Iliteremshwa ya 46 الواقعة 57 Al-Hadid AlHadid · aya 29 · Madina Juzuu 27 · Iliteremshwa ya 94 الحديد 58 Al-Mujadilah Al-Mujadalah · aya 22 · Madina Juzuu 28 · Iliteremshwa ya 105 المجادلة 59 Al-Hashr aya 24 · Madina Juzuu 28 · Iliteremshwa ya 101 الحشر 60 Al-Mumtahinah Al-Mumtahanah · aya 13 · Madina Juzuu 28 · Iliteremshwa ya 91 الممتحنة 61 As-Saff aya 14 · Madina Juzuu 28 · Iliteremshwa ya 109 الصف 62 Al-Jumu'ah Al-Juma'ah · aya 11 · Madina Juzuu 28 · Iliteremshwa ya 110 الجمعة 63 Al-Munafiqun Al-Munafikun · aya 11 · Madina Juzuu 28 · Iliteremshwa ya 104 المنافقون 64 At-Taghabun aya 18 · Madina Juzuu 28 · Iliteremshwa ya 108 التغابن 65 At-Talaq At-Talak · aya 12 · Madina Juzuu 28 · Iliteremshwa ya 99 الطلاق 66 At-Tahrim aya 12 · Madina Juzuu 28 · Iliteremshwa ya 107 التحريم 67 Al-Mulk aya 30 · Makka Juzuu 29 · Iliteremshwa ya 77 الملك 68 Al-Qalam Al-Kalam · aya 52 · Makka Juzuu 29 · Iliteremshwa ya 2 القلم 69 Al-Haqqah Al-Hakkah · aya 52 · Makka Juzuu 29 · Iliteremshwa ya 87 الحاقة 70 Al-Ma'arij aya 44 · Makka Juzuu 29 · Iliteremshwa ya 79 المعارج 71 Nooh Nouh · aya 28 · Makka Juzuu 29 · Iliteremshwa ya 71 نوح 72 Al-Jinn aya 28 · Makka Juzuu 29 · Iliteremshwa ya 40 الجن 73 Al-Muzzammil aya 20 · Makka Juzuu 29 · Iliteremshwa ya 3 المزمل 74 Al-Muddaththir Al-Muddasir · aya 56 · Makka Juzuu 29 · Iliteremshwa ya 4 المدثر 75 Al-Qiyamah Al-Kiyama · aya 40 · Makka Juzuu 29 · Iliteremshwa ya 31 القيامة 76 Al-Insan aya 31 · Madina Juzuu 29 · Iliteremshwa ya 98 الإنسان 77 Al-Mursalat aya 50 · Makka Juzuu 29 · Iliteremshwa ya 33 المرسلات 78 An-Naba' An-Naba'i · aya 40 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 80 النبأ 79 An-Nazi'at aya 46 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 81 النازعات 80 'Abasa Abasa · aya 42 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 24 عبس 81 At-Takwir An-Takwir · aya 29 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 7 التكوير 82 Al-Infitar aya 19 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 82 الإنفطار 83 Al-Mutaffifin aya 36 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 86 المطففين 84 Al-Inshiqaq Al-Inshikak · aya 25 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 83 الإنشقاق 85 Al-Buruj aya 22 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 27 البروج 86 At-Tariq At-Tarik · aya 17 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 36 الطارق 87 Al-A'la Al'A'alah · aya 19 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 8 الأعلى 88 Al-Ghashiyah aya 26 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 68 الغاشية 89 Al-Fajr aya 30 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 10 الفجر 90 Al-Balad aya 20 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 35 البلد 91 Ash-Shams As-Shams · aya 15 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 26 الشمس 92 Al-Lail aya 21 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 9 الليل 93 Ad-Duha Ad-Dhuhah · aya 11 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 11 الضحى 94 Ash-Sharh As-Sarhi · aya 8 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 12 الشرح 95 At-Tin aya 8 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 28 التين 96 Al-'Alaq Al'Alak · aya 19 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 1 العلق 97 Al-Qadr Al-Kadr · aya 5 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 25 القدر 98 Al-Baiyinah Al-Bayyinah · aya 8 · Madina Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 100 البينة 99 Az-Zalzalah Al-zalzalah · aya 8 · Madina Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 93 الزلزلة 100 Al-'Adiyat Al-Adiyat · aya 11 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 14 العاديات 101 Al-Qari'ah Al-Kari'ah · aya 11 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 30 القارعة 102 At-Takathur At-Takasur · aya 8 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 16 التكاثر 103 Al-'Asr Al'asri · aya 3 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 13 العصر 104 Al-Humazah Ali-Humazah · aya 9 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 32 الهمزة 105 Al-Fil aya 5 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 19 الفيل 106 Quraish Kuraish · aya 4 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 29 قريش 107 Al-Ma'un aya 7 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 17 الماعون 108 Al-Kauthar Al-Kausar · aya 3 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 15 الكوثر 109 Al-Kafirun aya 6 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 18 الكافرون 110 An-Nasr aya 3 · Madina Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 114 النصر 111 Al-Masad aya 5 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 6 المسد 112 Al-Ikhlas aya 4 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 22 الإخلاص 113 Al-Falaq Al-Flak · aya 5 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 20 الفلق 114 An-Nas aya 6 · Makka Juzuu 30 · Iliteremshwa ya 21 الناس

Mipangilio ya kusoma

Mwonekano
Linganisha na

Chagua hadi tafsiri mbili zaidi za kuonyesha chini ya kila aya.

Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Nafasi ya mistari
Mandhari

Aya

Tafsiri ya Kiarabu
Angazia

Uangaziaji unabaki kwenye kivinjari hiki na unaorodheshwa kwenye ukurasa wa alamisho. /bookmarks