قُلۡ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِن كُنتُمۡ فِي شَكّٖ مِّن دِينِي فَلَآ أَعۡبُدُ ٱلَّذِينَ تَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلَٰكِنۡ أَعۡبُدُ ٱللَّهَ ٱلَّذِي يَتَوَفَّىٰكُمۡۖ وَأُمِرۡتُ أَنۡ أَكُونَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Sema: Enyi watu! Ikiwa nyinyi mnayo shaka katika Dini yangu, basi mimi siwaabudu mnao waabudu nyinyi badala ya Mwenyezi Mungu. Lakini mimi namuabudu Mwenyezi Mungu anaye kufisheni. Na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waumini.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Sema, ewe Mtume, kuwaambia watu hawa, «Iwapo muko kwenye shaka juu ya usawa wa Dini yangu ambayo nimewaitia kwayo, nayo ni Uislamu, na juu ya uthabiti wangu na kujikita kwangu juu yake, pamoja ya kuwa nyinyi muna matumaini ya kuniepusha nayo, basi mimi sitamuabudu katika hali yoyote ile, yoyote miongoni mwa wale mnaowaabudu mkajifanyia masanamu na mizimu, lakini namuabudu Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Mwenye kuwafisha na kuzitwaa roho zenu, na nimeamrishwa niwe ni miongoni mwa wenye kumuamini na wenye kufuata Sheria Zake kivitendo.»
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس