قَدۡ خَسِرَ ٱلَّذِينَ قَتَلُوٓاْ أَوۡلَٰدَهُمۡ سَفَهَۢا بِغَيۡرِ عِلۡمٖ وَحَرَّمُواْ مَا رَزَقَهُمُ ٱللَّهُ ٱفۡتِرَآءً عَلَى ٱللَّهِۚ قَدۡ ضَلُّواْ وَمَا كَانُواْ مُهۡتَدِينَ
Hakika wamekhasirika wale ambao wamewauwa watoto wao kwa upumbavu pasipo kujua, na wakaharimisha alivyo waruzuku Mwenyezi Mungu kwa kumzulia Mwenyezi Mungu. Hakika wamepotea, wala hawakuwa wenye kuongoka.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Hakika wamepata hasara na wameangamia wale ambao, kwa udhaifu wa akili zao na kwa ujinga wao, waliwaua watoto wao na wakaziharamisha, kwa kumzulia Mwenyezi Mungu urongo, zile Alizowaruzuku. Wako mabali na haki na hawakuwa ni miongoni mwa watu wa uongofu na muelekeo wa sawa. Kuhalalisha na kuharamisha ni miongoni mwa mambo mahususi ya uungu katika uwekaji sheria. Halali ni Aliyoihalalisha Mwenyezi Mungu, na haramu ni Aliyoiharamisha Mwenyezi Mungu. Na haipasii kwa yoyote kati ya viumbe wake, awe mmoja au kundi, kuwaekea sheria waja Wake ambayo Mwenyezi Mungu Hakuidhinisha.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس