ثُمَّ ءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡكِتَٰبَ تَمَامًا عَلَى ٱلَّذِيٓ أَحۡسَنَ وَتَفۡصِيلٗا لِّكُلِّ شَيۡءٖ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٗ لَّعَلَّهُم بِلِقَآءِ رَبِّهِمۡ يُؤۡمِنُونَ
Tena tulimpa Musa Kitabu kwa kumtimizia (neema) aliye fanya wema, na kuwa ni maelezo ya kila kitu, na uwongofu na rehema, ili wapate kuamini mkutano wao na Mola wao Mlezi.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Kisha sema, ewe Mtume, uwaambie hawa washirikina, «Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Ndiye Aliyempa Mūsā Taurati, kwa kuzitimiza neema Zake kwa watu wa mila yake wanaofanya wema, na kwa kufafanua kila kitu katika mambo ya dini yao, na kuwapa uongofu na muelekeo wa njia iliyolingana sawa, na kuwarehemu, kwa matumaini kuwa watakubali kwamba kuna kufufuliwa baada ya kufa na kuna hesabu na malipo, na hilo liwafanya watende mema.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس