قُلۡ بِفَضۡلِ ٱللَّهِ وَبِرَحۡمَتِهِۦ فَبِذَٰلِكَ فَلۡيَفۡرَحُواْ هُوَ خَيۡرٞ مِّمَّا يَجۡمَعُونَ
Sema: Kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake! Basi nawafurahi kwa hayo. Haya ni bora kuliko hayo wanayo yakusanya.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Sema, ewe Mtume, kuwaambia watu wote, «Kwa wema wa Mwenyezi Mungu na rehema Yake, basi na wawe na furaha.» Wema wa Mwenyezi mungu na rehema Yake ni Uislamu ambao ni uongofu na ni Dini ya haki aliyokuja nayo Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kwani Uislamu ambao Mwenyezi Mungu Amewaita wao waufuate, na Qur’ani ambayo Aliiteremsha kwa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye ni bora kuliko taka za ulimwengu wanazozikusanya na anasa zilizomo ndani yake zenye kutoeka kuondoka.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس