۞مَّآ أَشۡهَدتُّهُمۡ خَلۡقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَلَا خَلۡقَ أَنفُسِهِمۡ وَمَا كُنتُ مُتَّخِذَ ٱلۡمُضِلِّينَ عَضُدٗا
Sikuwashuhudisha kuumbwa kwa mbingu na ardhi, wala kuumbwa kwa nafsi zao. Wala sikuwafanya wapotezao kuwa ni wasaidizi.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Sikumleta Iblisi na kizazi chake, ambao nyinyi mnawatii, katika uumbaji wa mbingu na ardhi, nikataka msaada wao kuziumba, wala sikuwashuhudisha baadhi yao uumbaji wa wengine. Bali mimi nilipwekeka katika kuumba zote hizo bila msaidizi wala mwenye kutilia nguvu, na sikuwa ni mwenye kuwafanya wapotezaji miongoni mwa Mashetani na wengineo kuwa ni wasaidizi, basi vipi nyinyi mnawapatia haki yangu na mnawafanya wao ni wategemewa wenu badala yangu na hali mimi ndiye muumba wa kila kitu.?
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس