وَإِذَآ أَذَقۡنَا ٱلنَّاسَ رَحۡمَةٗ فَرِحُواْ بِهَاۖ وَإِن تُصِبۡهُمۡ سَيِّئَةُۢ بِمَا قَدَّمَتۡ أَيۡدِيهِمۡ إِذَا هُمۡ يَقۡنَطُونَ
Na watu tunapo waonjesha rehema huifurahia, na ukiwasibu uovu kwa iliyo yatanguliza mikono yao wenyewe, mara wanakata tamaa.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na tunapowaonjesha watu neema itokayo kwetu ya afya, uzima na mafanikio, wanafurahia hilo furaha ya kiburi na majivuno, na sio furaha ya shukrani. Na yakiwapata wao magonjwa, umasikini, kuogopa na dhiki kwa sababu ya dhambi zao na maasia yao, ghafula wao wanakata tamaa kuwa hayo yatawaondokea. Na hii ni tabia ya wengi wa watu katika hali ya neema na matatizo.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس