وَلَوۡ أَنَّ لِكُلِّ نَفۡسٖ ظَلَمَتۡ مَا فِي ٱلۡأَرۡضِ لَٱفۡتَدَتۡ بِهِۦۗ وَأَسَرُّواْ ٱلنَّدَامَةَ لَمَّا رَأَوُاْ ٱلۡعَذَابَۖ وَقُضِيَ بَيۡنَهُم بِٱلۡقِسۡطِ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ
Na lau kuwa kila nafsi iliyo dhulumu inamiliki kila kiliomo duniani, bila ya shaka ingeli toa vyote kujikombolea. Na watakapo iona adhabu wataficha majuto. Na patahukumiwa baina yao kwa uadilifu, nao hawatadhulumiwa.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na lau kwamba kila nafsi iliyomshirikisha na kumkanusha Mwenyezi Mungu itakuwa na vyote vilivyomo ardhini, na ikamkinika kuvifanya ni fidia yake ya kujikomboa na adhabu hiyo, ingalijikomboa kwavyo. Na wale ambao walidhulumu wataficha majuto yao watakapoiona adhabu ya Mwenyezi Mungu imewashukia wao wote. Na Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kuwa juu, Atahukumu baina yao kwa uadilifu, na wao hawatadhulumiwa, kwa kuwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, Hamuadhibu yoyote isipokuwa kwa dhambi zake.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس