فَإِن كُنتَ فِي شَكّٖ مِّمَّآ أَنزَلۡنَآ إِلَيۡكَ فَسۡـَٔلِ ٱلَّذِينَ يَقۡرَءُونَ ٱلۡكِتَٰبَ مِن قَبۡلِكَۚ لَقَدۡ جَآءَكَ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُمۡتَرِينَ
Na ikiwa unayo shaka katika tuliyo kuteremshia, basi waulize wasomao Kitabu kabla yako. Kwa yakini imekwisha kujia Haki kutoka kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wenye shaka.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Basi uwapo na shaka,ewe Mtume, juu ya ukweli wa yale tuliyokupa habari yake, waulize wanaosoma Kitabu kabla yako miongoni mwa watu wa Taurati na Injili. Kwani hilo limethibiti kwenye vitabu vyao. Hakika umejiwa na ukweli wa yakini, kutoka kwa Mola wako, kwamba wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na kwamba hawa Mayahudi na Wanaswara wanajua ukweli wa hilo na wanapata sifa zako katika vitabu vyao, lakini wao wanalikataa hilo pamoja na kuwa walijua. Basi usiwe ni miongoni mwa wenye kufanya shaka juu ya usawa wa hilo na ukweli wake. Makusudio ya aya hii ni kusimamisha hoja kwa washirikina kwa ushahidi wa Watu wa Kitabu kati ya Wayahudi na Wanaswara ili kuukata udhuru wao.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس