وَرَبُّكَ ٱلۡغَنِيُّ ذُو ٱلرَّحۡمَةِۚ إِن يَشَأۡ يُذۡهِبۡكُمۡ وَيَسۡتَخۡلِفۡ مِنۢ بَعۡدِكُم مَّا يَشَآءُ كَمَآ أَنشَأَكُم مِّن ذُرِّيَّةِ قَوۡمٍ ءَاخَرِينَ
Na Mola wako Mlezi ndiye Mkwasi, Mwenye rehema. Akipenda atakuondoeni na awaweke wengine awapendao badala yenu, kama vile alivyo kutoeni kutokana na uzazi wa watu wengine.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na Mola wako, ewe Mtume, Aliyewaamrisha watu kumuabudu, Ndiye Mkwasi Peke Yake, na viumbe wote wanamhitajia Yeye. Na Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye Mwenye rehema kunjufu. Na lau Alitaka Angaliwaangamiza na Akawaleta watu wengine wasiokuwa nyinyi watakaokuwa badala yenu baada ya kumalizika kwenu na watende matendo ya kumtii Yeye, Aliyetukuka, kama Alivyowaleta nyinyi kutokamana na kizazi cha watu wengine waliokuwako kabla yenu.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس