قُل لَّآ أَقُولُ لَكُمۡ عِندِي خَزَآئِنُ ٱللَّهِ وَلَآ أَعۡلَمُ ٱلۡغَيۡبَ وَلَآ أَقُولُ لَكُمۡ إِنِّي مَلَكٌۖ إِنۡ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰٓ إِلَيَّۚ قُلۡ هَلۡ يَسۡتَوِي ٱلۡأَعۡمَىٰ وَٱلۡبَصِيرُۚ أَفَلَا تَتَفَكَّرُونَ
Sema: Mimi sikwambiini kuwa ninazo khazina za Mwenyezi Mungu. Wala sijui mambo yaliyo fichikana. Wala sikwambiini kuwa mimi ni Malaika. Mimi sifuati ila yanayo funuliwa kwangu. Sema: Je, wanakuwa sawa, kipofu na mwenye kuona. Basi hamfikiri?
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Sema, ewe Mtume, kuwaambia washirikina hawa, «Mimi sidai kuwa ninamiliki hazina za mbingu na ardhi nikawa ninazitumia nitakavyo; na sidai kuwa mimi najua al-ghayb (yasiyoonekana); na sidai kuwa mimi ni Malaika. Mimi ni Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu, nafuata yale nliyoteremshiwa kwa njia ya wahyi na nawafikishia watu wahyi Wake.» Waambie, ewe Mtume, washirikina hawa. «Je, kafiri aliye kipofu wa kutoziona aya za Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, asiziamini yuko sawa na Muumini anayeziona aya za Mwenyezi Mungu na akaziamini? Kwani nyinyi hamuzifikirii aya za Mwanye ili muione haki na muiamini?»
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس