وَأَنذِرۡ بِهِ ٱلَّذِينَ يَخَافُونَ أَن يُحۡشَرُوٓاْ إِلَىٰ رَبِّهِمۡ لَيۡسَ لَهُم مِّن دُونِهِۦ وَلِيّٞ وَلَا شَفِيعٞ لَّعَلَّهُمۡ يَتَّقُونَ
Na waonye kwayo wanao ogopa kuwa watakusanywa kwa Mola wao Mlezi, hali kuwa hawana mlinzi wala mwombezi isipo kuwa Yeye, ili wapate kuchamngu.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na watishe, ewe Mtume, kwa hii Qur’ani wale ambao wanajua kuwa wao watafufuliwa wapelekwe kwa Mola wao. Wao wanaiyamini ahadi ya Mwenyezi Mungu ya kuwalipa mema wenye kufanya wema na kuwalipa maovu wenye kufanya uovu. Wao hawana, isipokuwa Mwenyezi Mungu, mtegemewa mwenye kuwanusuru wala muombezi mwenye kuwaombea mbele Yake Aliyetukuka Akawaokoa na adhabu Yake. Kwani huenda wao wakamcha Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kwa kuyafanya maamrisho na kuyaepuka makatazo.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس