ذَٰلِكَ هُدَى ٱللَّهِ يَهۡدِي بِهِۦ مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦۚ وَلَوۡ أَشۡرَكُواْ لَحَبِطَ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Hiyo ni hidaya ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo humhidi amtakaye katika waja wake. Na lau wangeli mshirikisha yangeli waharibikia waliyo kuwa wakiyatenda.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Uongofu huo ni taufiki ya Mwenyezi Mungu ambayo kwayo Anamuongoza Anayemtaka miongoni mwa waja Wake. Na lau hawa Manabii walimshirikisha Mwenyezi Mungu, kwa kuchukulia na kukadiria, amali zao zingalipomoka. Kwani Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Hakubali amali yoyote pamoja na ushirikina.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس