وَلَا تَسُبُّواْ ٱلَّذِينَ يَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ فَيَسُبُّواْ ٱللَّهَ عَدۡوَۢا بِغَيۡرِ عِلۡمٖۗ كَذَٰلِكَ زَيَّنَّا لِكُلِّ أُمَّةٍ عَمَلَهُمۡ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّهِم مَّرۡجِعُهُمۡ فَيُنَبِّئُهُم بِمَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Wala msiwatukane hao wanao waomba badala ya Mwenyezi Mungu, wasije na wao wakamtukana Mwenyezi Mungu kwa jeuri bila ya kujua. Namna hivyo tumewapambia kila umma vitendo vyao. Kisha marejeo yao yatakuwa kwa Mola wao Mlezi, naye atawaambia waliyo kuwa wakiyatenda.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na msiyatukane, enyi Waislamu, masanamu ambyo washirikina wanayaabudu, kwa ajili ya kuziba kipengele, ili hilo lisije likawafanya wao wamtukane Mwenyezi Mungu kwa ujinga na kwa uadui, bila ya kuwa na ujuzi. Na kama tulivyowapambia hawa matendo yao mabaya, yakiwa ni mateso kwao kwa uchaguzi wao mbaya, ndivyo tulivyowapambia kila umma matendo yao. Kisha marejeo yao wote ni kwa Mola wao; hapo Mwenyezi Mungu Awaambie matendo yao waliokuwa wakiyatenda ulimwenguni kisha Awalipe kwayo.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس