وَمِنَ ٱلۡإِبِلِ ٱثۡنَيۡنِ وَمِنَ ٱلۡبَقَرِ ٱثۡنَيۡنِۗ قُلۡ ءَآلذَّكَرَيۡنِ حَرَّمَ أَمِ ٱلۡأُنثَيَيۡنِ أَمَّا ٱشۡتَمَلَتۡ عَلَيۡهِ أَرۡحَامُ ٱلۡأُنثَيَيۡنِۖ أَمۡ كُنتُمۡ شُهَدَآءَ إِذۡ وَصَّىٰكُمُ ٱللَّهُ بِهَٰذَاۚ فَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبٗا لِّيُضِلَّ ٱلنَّاسَ بِغَيۡرِ عِلۡمٍۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ
Na wawili katika ngamia, na wawili katika ng'ombe. Sema: Je, ameharimisha yote madume wawili au majike wawili, au waliomo matumboni mwa yote majike? Au, nyinyi mlikuwapo Mwenyezi Mungu alipo kuusieni haya? Basi ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule aliye mzulia Mwenyezi Mungu uwongo, kwa ajili ya kuwapoteza watu bila ya ilimu? Hakika Mwenyezi Mungu hawahidi watu madhaalimu.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na aina nne nyingine ni aina mbili za ngamia, waume na wake, na aina mbili za ng’ombe, waume na wake. Sema, ewe Mtume, kuwaambia washirikina hao, «Kwani Mwenyezi Mungu Amewaharamisha madume wawili au majike wawili? Au Ameharamisha vilivyomo ndani ya matumbo ya majike wawili, wawe madume au majike? Au mlikuwa, enyi washirikina, mupo pindi Mwanyezi Mungu Alipowapa wasia wa uharamu huu wa wanyama howa? Hakuna dhalimu mbaya zaidi kuliko yule aliyemzulia Mwenyezi Mungu urongo, ili awapotoshe watu, kwa ujinga wake, na njia ya uongofu. Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Hamuelekezi kwenye muelekeo wa sawa yule aliyekiuka mpaka wake, akamzulia urongo Mola wake na akawapoteza watu.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس