قُلۡ مَن يَرۡزُقُكُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِ أَمَّن يَمۡلِكُ ٱلسَّمۡعَ وَٱلۡأَبۡصَٰرَ وَمَن يُخۡرِجُ ٱلۡحَيَّ مِنَ ٱلۡمَيِّتِ وَيُخۡرِجُ ٱلۡمَيِّتَ مِنَ ٱلۡحَيِّ وَمَن يُدَبِّرُ ٱلۡأَمۡرَۚ فَسَيَقُولُونَ ٱللَّهُۚ فَقُلۡ أَفَلَا تَتَّقُونَ
Sema: Ni nani anaye kuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Au ni nani anaye miliki kusikia na kuona? Na nani amtoaye hai kutoka maiti, na akamtoa maiti kutoka aliye hai? Na nani anaye yadabiri mambo yote? Watasema: Allah, Mwenyezi Mungu. Basi sema: Je! Hamchi?
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Waambie, ewe Mtume, washirikina hawa, «Ni nani anayewaruzuku kutoka juu kwa mvua anayoiteremsha, na kutoka ardhini kwa mimea na miti aina mbalimabali anayoiotesha kutoka humo, ambayo miongoni mwayo mnakula nyinyi na wanyama wenu? Na ni nani anayemiliki hisia za kusikia na za kuona mnazostarehea, nyinyi na wengineo? Na ni nani anayemiliki uhai na kifo, katika ulimwengu wote, akawatoa wenye uhai na wafu, baadhi yao kutoka kwa wengine, katika viumbe mnavyovijua na msivyovijua? Na ni nani anayeyaendesha mambo ya mbinguni na ardhini na yaliyomo ndani yake, (anayeyaendesha) mambo yenu nyinyi na mambo ya viumbe vyote?» Watakujibu kwamba anayefanya yote hayo ni Mwenyezi Mungu. Waambie, «Basi si muogope mateso ya Mwenyezi Mungu mnapomuabudu mwingine pamoja na Yeye?»
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس