وَكَذَٰلِكَ زَيَّنَ لِكَثِيرٖ مِّنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ قَتۡلَ أَوۡلَٰدِهِمۡ شُرَكَآؤُهُمۡ لِيُرۡدُوهُمۡ وَلِيَلۡبِسُواْ عَلَيۡهِمۡ دِينَهُمۡۖ وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ مَا فَعَلُوهُۖ فَذَرۡهُمۡ وَمَا يَفۡتَرُونَ
Na kadhaalika hao washirika wao wamewapambia wengi katika washirikina kuwauwa watoto wao ili kuwaangamiza na kuwavurugia dini yao. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli penda wasinge fanya hayo. Basi waache na hayo wanayo yazua.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na kama ambavyo mashetani waliwapambia washirikina wamtengee Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, katika mazao na wanyama howa, fungu maalumu na fungu kwa washirika wao, vilevile mashetani wamewapambia wengi kati ya washirikina kuwaua watoto wao kwa kuchelea ufukara, ili wawaingize wazazi hawa kwenye maangamivu kwa kuziua nafsi ambazo Mwenyezi Mungu Ameharamisha kuuliwa isipokuwa kwa haki, na ili wawavurugie dini yao iwachanganyikie wapate kupotea na waangamie. Na lau Angalitaka Mwenyezi Mungu wasiifanye hilo hawangalilifanya, lakini Yeye Amelikadiria liwe kwa kujua Kwake uovu wa hali yao na marejeo yao. Basi waache, ewe Mtume, na mambo yao, katika yale ya urongo wanayoyazua , na Mwenyezi Mungu Atahukumu baina yako na wao.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس