قُلۡ هَلُمَّ شُهَدَآءَكُمُ ٱلَّذِينَ يَشۡهَدُونَ أَنَّ ٱللَّهَ حَرَّمَ هَٰذَاۖ فَإِن شَهِدُواْ فَلَا تَشۡهَدۡ مَعَهُمۡۚ وَلَا تَتَّبِعۡ أَهۡوَآءَ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا وَٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ وَهُم بِرَبِّهِمۡ يَعۡدِلُونَ
Sema: Leteni mashahidi wenu watao shuhudia kuwa Mwenyezi Mungu ameharimisha hawa. Basi wakishuhudia, wewe usishuhudie pamoja nao. Wala usifuate matamanio ya walio zikanusha Ishara zetu, wala hawaiamini Akhera, na ambao wanamlinganisha Mola Mlezi wao na wengine.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, «Waleteni mashahidi wenu ambao watatoa ushahidi kwamba Mwenyezi Mungu Ndiye Aliyeharamisha vile mlivyoviharamisha vya makulima na wanyama howa.» Wakitoa ushahidi huo, kwa urongo na uzushi, usiwaamini wala usikubaliane na wale waliojitolea uamuzi wenyewe kulingana na mapendeleo ya nafsi zao, wakazikanusha aya za Mwenyezi Mungu katika yale waliyoyashikilia ya kukiharamisha Alichokihalalisha Mwenyezi Mungu na kukihalalisha Alichokiharamisha Mwenyezi Mungu. Wala usiwafuate wale ambao hawayaamini maisha ya Akhera wala wasiotenda vitendo vya kuwafaa huko na wale ambao Mola wao wanamshirikisha wakawa wanamuabudu mwingine pamoja na Yeye.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس