قُلۡ أَنَدۡعُواْ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَنفَعُنَا وَلَا يَضُرُّنَا وَنُرَدُّ عَلَىٰٓ أَعۡقَابِنَا بَعۡدَ إِذۡ هَدَىٰنَا ٱللَّهُ كَٱلَّذِي ٱسۡتَهۡوَتۡهُ ٱلشَّيَٰطِينُ فِي ٱلۡأَرۡضِ حَيۡرَانَ لَهُۥٓ أَصۡحَٰبٞ يَدۡعُونَهُۥٓ إِلَى ٱلۡهُدَى ٱئۡتِنَاۗ قُلۡ إِنَّ هُدَى ٱللَّهِ هُوَ ٱلۡهُدَىٰۖ وَأُمِرۡنَا لِنُسۡلِمَ لِرَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Sema: Je, tumuombe asiye kuwa Mwenyezi Mungu ambae hatufai wala hatudhuru, na turejee nyuma baada ya Mwenyezi Mungu kwisha tuhidi? Tuwe kama ambao mashet'ani wamempumbaza katika ardhi, amebabaika? Anao marafiki wanao mwita ende kwenye uwongofu, wakimwambia: Njoo kwetu! Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio Uwongofu. Nasi tumeamrishwa tusilimu kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote,
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, «Je, tuabudu, asiyekuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, masanamu yasionufaisha wala kudhuru? Je, turudi ukafirini baada ya Mwenyezi Mungu kutuongoza kwenye Uislamu, tukafanana, katika kurudi kwetu ukafirini, na aliyeharibika akili yake kwa kusawazwa na mashetani akapotea njia ardhini na hali yeye ana marafiki wenye akili, wenye Imani, wamwita kwenye njia ya sawa ambayo wao wako akawa anakataa?» Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, «Uongofu wa Mwenyezi Mungu Aliyenituma mimi ndio uongofu wa haki. Na sote tumeamrishwa tujisalimishe kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Bwana wa vuimbe vyote, kwa kumuabudu, Peke Yake, Asiye na mshirika, kwani Yeye Ndiye Mola na Mmiliki wa kila kitu.»
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس