فَلَوۡلَا كَانَ مِنَ ٱلۡقُرُونِ مِن قَبۡلِكُمۡ أُوْلُواْ بَقِيَّةٖ يَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلۡفَسَادِ فِي ٱلۡأَرۡضِ إِلَّا قَلِيلٗا مِّمَّنۡ أَنجَيۡنَا مِنۡهُمۡۗ وَٱتَّبَعَ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ مَآ أُتۡرِفُواْ فِيهِ وَكَانُواْ مُجۡرِمِينَ
Basi mbona hawakuwamo katika watu wa kabla yenu wenye vyeo na wasaa wanao kataza uharibifu katika nchi, isipo kuwa wachache tu, ambao ndio tulio waokoa? Na walio dhulumu walifuata starehe zao, na wakawa ni wakosefu.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Si ilikuwa wapatikane, miongoni mwa vizazi viliyopita kabla yenu, wasalia wa watu wazuri walio wema wanaowakataza makafiri waache ukafiri wao na kufanya uharibifu katika ardhi. Hawakupatikana katika hao isipokuwa wachache miongoni mwa walioamini na Mwenyezi Mungu akawaokoa na adhabu Yake Alipowapatiliza madhalimu. Na waliozidhulumu nafsi zao, miongoni mwa watu wa kila ummah uliopita, walifuata ladha za duniani na anasa zake walizostareheshwa, na wakawa wahalifu, wenye kudhulumu kwa kufuata kwao starehe walizokuwa nazo, ndipo adhabu ikathibiti juu yao. Katika hii aya pana mazingatio na mawaidha kwa wanaofanya maasia miongoni mwa Waislamu, kwa kuwa hawaepukani na udhalimu wa nafsi zao.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس