أَوۡ تَقُولُواْ لَوۡ أَنَّآ أُنزِلَ عَلَيۡنَا ٱلۡكِتَٰبُ لَكُنَّآ أَهۡدَىٰ مِنۡهُمۡۚ فَقَدۡ جَآءَكُم بَيِّنَةٞ مِّن رَّبِّكُمۡ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٞۚ فَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّن كَذَّبَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ وَصَدَفَ عَنۡهَاۗ سَنَجۡزِي ٱلَّذِينَ يَصۡدِفُونَ عَنۡ ءَايَٰتِنَا سُوٓءَ ٱلۡعَذَابِ بِمَا كَانُواْ يَصۡدِفُونَ
Au mkasema: Lau kuwa tumeteremshiwa sisi Kitabu tungeli kuwa waongofu zaidi kuliko wao. Basi imekufikieni bayana kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na uwongofu, na rehema. Basi nani aliye dhaalimu mkubwa zaidi kuliko yule anaye kanusha Ishara za Mwenyezi Mungu, na akajitenga nazo? Tutawalipa wanao jitenga na Ishara zetu adhabu kali kabisa kwa sababu ya kujitenga kwao.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na ili msije mkasema, enyi washirikina, «Lau kama sisi tuliteremshiwa kitabu kutoka mbinguni, kama walivyoteremshiwa Mayahudi na Wanaswara, tungalikuwa na muelekeo madhubuti sana kwenye njia ya haki kuliko wao.» Hakika kimewajia Kitabu kwa lugha ya Kiarabu chenye ufafanuzi. Na hiyo ni hoja iliyo wazi kutoka kwa Mola wenu, ni muongozo wa njia ya haki na ni rehema kwa umma huu. Na hapana yoyote mbaya wa dhuluma na uadui kuliko yule aliyezikanusha hoja za Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na akazipa mgongo. Basi hawa wenye kupa mgongo tutawatesa mateso makubwa kwenye Moto wa Jahanamu, kwa sababu ya kuzipa mgongo kwao aya zetu na kuzuia kwao njia zetu.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس