فَلَعَلَّكَ تَارِكُۢ بَعۡضَ مَا يُوحَىٰٓ إِلَيۡكَ وَضَآئِقُۢ بِهِۦ صَدۡرُكَ أَن يَقُولُواْ لَوۡلَآ أُنزِلَ عَلَيۡهِ كَنزٌ أَوۡ جَآءَ مَعَهُۥ مَلَكٌۚ إِنَّمَآ أَنتَ نَذِيرٞۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ وَكِيلٌ
Basi labda utaacha baadhi ya yale yaliyo funuliwa kwako, na kifua kitaona dhiki kwa hayo, kwa sababu wanasema: Mbona hakuteremshiwa khazina, au wakaja naye Malaika? Wewe ni mwonyaji tu, na Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wa kila kitu.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Huenda wewe, ewe Mtume, kwa ukafiri na ukanushaji mkubwa unaouona kwao, ukawa ni mwenye kuyaacha baaadhi ya yale unaoyoletewa wahyi kati ya yale ambayo Mwenyezi Mungu Alikuteremshia na Akakuamuru kuyafikisha, na kifua chako kikawa ni chenye kuhisi dhiki kwa hayo, kwa kuogopa wasije wakataka baadhi ya mambo kutoka kwako kwa njia ya kukusumbua, kama vile kusema, «Kwa nini asiteremshiwe mali mengi, au asijiwe na Malaika ambaye atamuamini katika ujumbe wake?» Basi wafikishie yale niliyokuletea wahyi kwayo, kwani lako wewe si lingine isipokuwa ni kuonya kwa yale uliyoletewa wahyi. Na Mwenyezi Mungu ni Mtunzi wa kila kitu, Anaendesha mambo yote ya viumbe vyake.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس