تِلۡكَ مِنۡ أَنۢبَآءِ ٱلۡغَيۡبِ نُوحِيهَآ إِلَيۡكَۖ مَا كُنتَ تَعۡلَمُهَآ أَنتَ وَلَا قَوۡمُكَ مِن قَبۡلِ هَٰذَاۖ فَٱصۡبِرۡۖ إِنَّ ٱلۡعَٰقِبَةَ لِلۡمُتَّقِينَ
Hizi ni katika khabari za ghaibu tunazo kufunulia. Hukuwa ukizijua wewe, wala watu wako, kabla ya hii. Basi subiri! Hakika Mwisho ni wa wachamngu.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Habari hiyo tuliyokuhadithia kuhusu Nūḥ na watu wake ni miongoni mwa habari za ghaibu zilizopita, ambazo tunakuletea wahyi juu yake, hukuwa ukizijua, wewe wala watu wako, kabla ya maelezo haya. Basi subiri juu ya ukanushaji wa watu wako na makero yao wanayokufanyia kama walivyosubiri Manabii huko nyuma. Na mwisho mwema wa duniani na Akhera ni wa waogopao wanaomcha Mwenyezi Mungu.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس