وَحَآجَّهُۥ قَوۡمُهُۥۚ قَالَ أَتُحَـٰٓجُّوٓنِّي فِي ٱللَّهِ وَقَدۡ هَدَىٰنِۚ وَلَآ أَخَافُ مَا تُشۡرِكُونَ بِهِۦٓ إِلَّآ أَن يَشَآءَ رَبِّي شَيۡـٔٗاۚ وَسِعَ رَبِّي كُلَّ شَيۡءٍ عِلۡمًاۚ أَفَلَا تَتَذَكَّرُونَ
Na watu wake wakamhoji. Akasema: Je, mnanihoji juu ya Mwenyezi Mungu, na hali Yeye ameniongoa? Wala siogopi hao mnao washirikisha naye, ila Mola wangu Mlezi akipenda kitu. Mola wangu Mlezi amekusanya ilimu ya kila kitu. Basi je, hamkumbuki?
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Watu wake walimjadili kuhusu kumpwekesha Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, akasema «Mwanijadili juu ya kumpwekesha kwangu Mwenyezi Mungu kwa ibada, na hali Yeye Ameniongoza nikaujua upweke Wake? Na iwapo nyinyi mnanitisha na waungu wenu wasije wakanidhuru, basi mimi siwaogopi na hawatanidhuru isipokuwa Mola wangu Atake jambo. Mola wangu Ameenea kila kitu kwa ujuzi. Basi hamkumbuki mkajua kuwa Yeye, Peke Yake, Ndiye Mstahiki wa kuabudiwa?
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس