وَهُوَ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٖ وَكَانَ عَرۡشُهُۥ عَلَى ٱلۡمَآءِ لِيَبۡلُوَكُمۡ أَيُّكُمۡ أَحۡسَنُ عَمَلٗاۗ وَلَئِن قُلۡتَ إِنَّكُم مَّبۡعُوثُونَ مِنۢ بَعۡدِ ٱلۡمَوۡتِ لَيَقُولَنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا سِحۡرٞ مُّبِينٞ
Na Yeye ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Na Kiti chake cha Enzi kilikuwa juu ya maji, ili akufanyieni mtihani ajuulikane ni nani miongoni mwenu mzuri zaidi wa vitendo. Na wewe ukisema: Nyinyi hakika mtafufuliwa baada ya kufa; wale walio kufuru husema: Hayakuwa haya ila ni uchawi uliyo wazi.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na Yeye Ndiye Ambaye Aliumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake kwa Siku Sita na Arshi Yake ilikuwa iko juu ya maji kabla ya hapo, Apate kuwajaribu nyinyi, ni nani kati yenu mzuri zaidi wa utiifu na utendaji. Utendaji wenye kumtakasia Mwenyezi Mungu, wenye kulingana na vile Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, alivyokuwa. Na lau unasema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina wa watu wako, «Nyinyi mtafufuliwa mkiwa hai baada ya kufa kwenu.» Watafanya haraka kukanusha na watasema, «Haikuwa hii Qur’ani unayotusomea isipokuwa ni uchawi ulio wazi.»
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس