وَقَالَ ٱلَّذِينَ أَشۡرَكُواْ لَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ مَا عَبَدۡنَا مِن دُونِهِۦ مِن شَيۡءٖ نَّحۡنُ وَلَآ ءَابَآؤُنَا وَلَا حَرَّمۡنَا مِن دُونِهِۦ مِن شَيۡءٖۚ كَذَٰلِكَ فَعَلَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۚ فَهَلۡ عَلَى ٱلرُّسُلِ إِلَّا ٱلۡبَلَٰغُ ٱلۡمُبِينُ
Na washirikina wanasema: Mwenyezi Mungu angeli taka tusingeli abudu chochote badala yake, sisi wala baba zetu, wala tusingeli harimisha chochote bila ya Yeye. Kama hivyo walifanya walio kuwa kabla yao. Basi lipo lolote juu ya Mitume isipo kuwa kubalighisha kwa uwazi?
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na washirikina walisema, «Lau kama Mwenyezi Mungu Alitaka tumuabudu Yeye Peke Yake, hatungalimuabudu yoyote asiyekuwa Yeye, sisi wala baba zetu kabla yetu, wala hatungaliharamisha chochote Asichokiharamisha». Ni hoja kama hizi za kipotofu walizozitumia makafifiri waliopita. Na wao ni warongo, kwani Mwenyezi Mungu Aliwaamrisha na Akawakataza na Akawawezesha kuyasimamia Aliyowakalifisha nayo, na Akawapa nguvu na matakwa yanayotokamana na vitendo vyao. Kwa hivyo, kujenga hoja kwao wakitegemea mapitisho ya Mwenyezi Mungu na makadirio Yake ni ubatilifu mkubwa baada ya kuonywa kwao na Mitume. Na Mitume wenye kuwaonya hawana la zaidi isipokuwa kuufikisha ujumbe ulio wazi waliokalifishwa nao.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس