وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ لَجَعَلَكُمۡ أُمَّةٗ وَٰحِدَةٗ وَلَٰكِن يُضِلُّ مَن يَشَآءُ وَيَهۡدِي مَن يَشَآءُۚ وَلَتُسۡـَٔلُنَّ عَمَّا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
Na Mwenyezi Mungu angeli taka, kwa yakini angeli kufanyeni umma mmoja. Lakini anamwachia kupotea anaye mtaka, na anamwongoa amtakaye. Na hakika mtaulizwa kwa yale mliyo kuwa mkiyafanya.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na lau Mwenyezi Mungu angalitaka angaliwaafikia nyote Akawafanya muwe kwenye muelekeo mmoja, nao ni Uislamu na Imani, na Angaliwalazimisha nao. Lakini Yeye, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, Anampoteza Anayemtaka, kati ya wale ambao Yeye Alijua kuwa walichagua upotevu, Asimuongoze kwa uadilifu Wake. Na Anamuongoza Anayemtaka, kati ya wale ambao Yeye Alijua kuwa wao walichagua haki, Akampa muelekeo kwa wema Wake. Na Mwenyezi Mungu Atawauliza nyinyi nyote, Siku ya Kiyama, yale ambayo mlikuwa mkiyafanya ulimwenguni kati ya yale Aliyowaamrisha nayo na Aliyowakataza, na Atawalipa nyinyi kwa hayo.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس