سورة العاديات

الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس

ترجمة معاني سورة العاديات باللغة السواحلية من كتاب الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس

الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس

آية رقم 1
Mwenyezi Mungu Anaapa kwa farasi wenye kwenda shoti katika njia Yake kumkabili adui, wakitoa sauti kwa kasi ya kukimbia. Haifai kwa kiumbe kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni ushirikina.
آية رقم 2
Na wenye kutoa cheche za moto kwa kwato zao ngumu wanapokimbia kwa kasi.
آية رقم 3
Wenye kushambulia maadui kipindi cha asubuhi.
آية رقم 5
Wakautia kati, kwa kuuzunguka kwa vipando vyao, mkusanyiko wa maadui.
آية رقم 6
Hakika binadamu ni mkanushaji sana neema za Mola wake.
آية رقم 9
Kwani binadamu hajui linalomngojea mbele yake, pindi Mwenyezi Mungu Atakapowatoa wafu makaburini waende kuhesabiwa na kulipwa?
آية رقم 10
Na (kwani yeye hajui) yakatolewa yaliyo ndani ya vifua: mema au maovu?.
آية رقم 11
Hakika Mola wao kwao na kwa amali zao, Siku Hiyo, ni Mtambuzi; hakuna chenye kufichamana Kwake.
تقدم القراءة