ترجمة معاني سورة القدر باللغة السواحلية من كتاب الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
آية رقم 1
ﭴﭵﭶﭷﭸ
ﭹ
Sisi Tumeiteremsha Qur’ani katika usiku wa cheo na utukufu , nao ni moja wa masiku ya mwezi wa Ramdhani.
آية رقم 2
ﭺﭻﭼﭽﭾ
ﭿ
Na nilipi liliokujulisha, ewe Mtume, ni upi usiku wa cheo na utukufu?
آية رقم 3
ﮀﮁﮂﮃﮄﮅ
ﮆ
Usiku wa cheo na utukufu ni bora fadhila zake kuliko fadhila za miezi elfu moja isiyokuwa usiku huo.
آية رقم 4
Usiku huo hushuka Malaika na Jibrili, amani iwashukie, kwa ruhusa ya Mola wao kwa kila jambo Alilolikadiria liwe mwaka huo.
آية رقم 5
ﮑﮒﮓﮔﮕ
ﮖ
Usiku huo wote ni amani, hakuna shari, mpaka kutokea alfajiri.
تقدم القراءة