ترجمة معاني سورة الفلق باللغة السواحلية من كتاب الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
آية رقم 1
ﭤﭥﭦﭧ
ﭨ
Sema, ewe Mtume, «Najilinda na kutaka hifadhi kwa Bwana wa asubuhi.
آية رقم 2
ﭩﭪﭫﭬ
ﭭ
«Kutokana na shari la viumbe na udhia wao
آية رقم 3
ﭮﭯﭰﭱﭲ
ﭳ
«Na shari la usiku wenye giza lingi ungiapo na ujikitapo na mashari na maudhi mbalimbali yaliyomo ndani yake.
آية رقم 4
ﭴﭵﭶﭷﭸ
ﭹ
«Na shari la wchawi wenye kupuliza kwenye mafundo wanayoyafunga kwa lengo la kuroga.
آية رقم 5
ﭺﭻﭼﭽﭾ
ﭿ
«Na shari la hasidi mwenye kutukia watu, anapowahusudu na kuwadhuru, kwa kutaka neema za Mwenyezi Mungu Aliyewaneemesha ziwaondokee.»
تقدم القراءة