سورة التكاثر

الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس

ترجمة معاني سورة التكاثر باللغة السواحلية من كتاب الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس

الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس

آية رقم 1
Kumewashughulisha kujifahiri kwa mali na watoto mkawacha kumtii Mwenyezi Mungu
آية رقم 2
Kujishughulisha kwenu na hilo kumeendelea mpaka mkawa makaburini na mkazikwa humo.
آية رقم 3
Siyo namna hii inatakiwa iwapumbaze kushindana kwa wingi wa mali. Itawadhihirikia kuwa Nyumba ya Akhera ni bora kwenu.
آية رقم 4
Kisha tahadharini mtajua mwisho mbaya wa kutojishughulisha na Akhera.
آية رقم 5
Siyo namna hii inatakiwa iwashughulishe kushindana kwa wingi wa mali.Lau mnajua kikweli, mngalirudi nyuma na mngaliangusiliza kuokoa nafsi zenu kutoka kwenye maangamivu.
تقدم القراءة