سورة العلق

الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس

ترجمة معاني سورة العلق باللغة السواحلية من كتاب الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس

الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس

آية رقم 1
Soma, ewe Nabii, Qur’ani uliyoteremshiwa ukianza kwa Jina la Mola wako Aliyepwekeka kwa kuumba.
آية رقم 2
Aliyemuumba kila binadamu kwa pande la damu nzito nyekundu.
آية رقم 3
Soma, ewe Nabii, kile ulichoteremshiwa, na Mola wako ni Mwingi wa wema, Mwingi wa ukarimu.
آية رقم 4
Aliyewafundisha viumbe vyake kuandika kwa kalamu.
آية رقم 5
Alimfundisha binadamu vitu ambavyo hakuwa akivijua. Akamtoa kwenye giza la ujinga, Akampeleka kwenye nuru ya elimu.
آية رقم 8
Basi, ajue kila mwenye kutupa mipaka kuwa mwisho atarudi kwa Mwenyezi Mungu Ambaye Atamlipa kila binadamu kwa alilolitenda.
آية رقم 9
Je, umeona ujeuri wa ajabu zaidi kuliko wa mtu huyu, Abu jahl,
آية رقم 10
Anayemkataza mja wetu, Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, anapomsalia Mola wake?
آية رقم 11
Waonaje iwapo mwenye kukatazwa kusali yuko uongofuni, vipi anamkataza?
آية رقم 12
Au iwapo anaamrisha mwigine kumcha Mungu, vipi anamkataza hilo?
آية رقم 13
Waonaje iwapo huyu mwenye kukataza anakanusha lile alinganiwalo kwalo na kulipa mgongo,
آية رقم 15
Basi mambo si kama anvyodai Abu Jahl. Na asipokomeka na ushindani alionao na udhia wake, Tutamshika upaa wake kwa nguvu na kumtia Motoni.
آية رقم 16
Upaa wake ni upaa wenye maneno ya urongo na vitendo vya makosa.
آية رقم 17
Basi na awalete, mtupaji mipaka huyu, watu wa baraza ili wamsaidiye.
آية رقم 18
Sisi Tutawaita Malaika wa adhabu.
آية رقم 19
Mambo si kama Abu Jahl anavyoyadhania. Yeye, ewe Mtume, hawezi kukufanya lolote la kukudhuru Usimfuate kwa lile alilokuitia la kuwa uache Swala, bali msujudie Mola wako na uwe karibu na Yeye kwa kujipendekeza Kwake kwa kumtii.
تقدم القراءة