سورة الناس

الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس

ترجمة معاني سورة النّاس باللغة السواحلية من كتاب الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس

الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس

آية رقم 1
Sema, ewe Mtume, «Ninajilinda na kutaka hifadhi kwa Bwana wa watu, Mwenye uweza, Peke Yake, wa kulirudisha shari lao.
آية رقم 2
«Mfalme wa watu, Mwenye kupeleka mambo yao yote Anavyotaka, Aliye Mkwasi kutowahitajia.
آية رقم 3
«Mola wa watu, Ambaye hapana mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye.
آية رقم 4
«Kutokana na udhia wa shetani ambaye hutia watu wasiwasi wanapoghafilika na hujificha atajwapo Mwenyezi Mungu.
آية رقم 6
«Miongoni mwa mashetani wa kijini na kibinadamu.»
تقدم القراءة