ترجمة معاني سورة الإخلاص باللغة السواحلية من كتاب الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
آية رقم 1
ﭑﭒﭓﭔ
ﭕ
Sema, ewe Mtume, «Yeye Ndiye Mwenyezi Mungu Aliyepwekeka kwa ustahiki wa kuabudiwa, uumbaji na utakatifu wa Majina na Sifa, Asiye na mshirika katika hayo.
آية رقم 2
ﭖﭗ
ﭘ
«Mwenyezi Mungu Ambaye Peke Yake Ndiye Mwenye kukusudiwa kwa kukidhi haja na matakwa.
آية رقم 3
ﭙﭚﭛﭜ
ﭝ
«Hana mwana wala mzazi wala mke.
آية رقم 4
ﭞﭟﭠﭡﭢ
ﭣ
«Wala hakuna yoyote katika viumbe Vyake mwenye kufanana wala kushabihiyana na Yeye katika Majina Yake, Sifa Zake wala vitendo Vyake.»
تقدم القراءة