ترجمة معاني سورة القيامة باللغة السواحلية من كتاب الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس
آية رقم 1
ﮊﮋﮌﮍ
ﮎ
Anaapa Mwenyezi Mungu kwa Siku ya Hesabu na Malipo,
آية رقم 2
ﮏﮐﮑﮒ
ﮓ
na Anaapa kwa nafsi yenye kuamini na kuchamungu, inayomlaumu mwenyewe kwa kuacha matendo ya utiifu na kufanya matendo yenye kuangamiza, kwamba watu watafufuliwa.
آية رقم 3
ﮔﮕﮖﮗﮘ
ﮙ
Je anadhanihuyu binadamu kafiri kuwa sisi hatutaweza kuikusanya mifupa yake baada ya kuwa mbalimbali.?
آية رقم 4
ﮚﮛﮜﮝﮞﮟ
ﮠ
Ndio! Tutaikusanya na tunaweza kufanya vidole vyake au ncha za vidole vyake- baada ya kuvikusanya na kuzioanisha- viwe kwenye umbo la sawasawa, kama vilivyokuwa kabla ya kufa.
آية رقم 5
ﮡﮢﮣﮤﮥ
ﮦ
Bali binadamu anakanusha kufufuliwa, anataka asalie kwenye kufanya ubaya kwa siku za mbeleni za maisha yake.
آية رقم 6
ﮧﮨﮩﮪ
ﮫ
Kafiri huyu huwa akiuliza, akiliona jambo la kusimama Kiyama kuwa liko mbali, «Ni lini Siku ya Kiyama?’
آية رقم 7
ﮬﮭﮮ
ﮯ
Basi macho yatakapoduwaa na yakashituka kwa kutishika na kile yalichokiona cha vituko vya Siku ya Kiyama,
آية رقم 8
ﮰﮱ
ﯓ
na ukafutika mwangaza wa mwezi,
آية رقم 9
ﯔﯕﯖ
ﯗ
na vikakusanywa jua na mwezi katika kukosa mwangaza, kikawa kila mojawapo ya hivyo viwili hakina mwangaza,
آية رقم 10
ﯘﯙﯚﯛﯜ
ﯝ
wakati huo binadamu atasema, «Pa kukimbilia ni wapi kuiepuka adhabu?»
آية رقم 11
ﯞﯟﯠ
ﯡ
Mambo sivyo kama unavyotamani yawe, ewe binadamu, ya kutaka kukimbia. Huna mahali pa kukimbilia wala pa kupata uokozinfsi yake.
آية رقم 12
ﯢﯣﯤﯥ
ﯦ
Kwa Mwenyezi Mungu Peke Yake ndio mwisho wa viumbe Siku ya Kiyama na ndipo mahali pao pa kutulia, na hapo Amlipe kila mtu kwa kile alichostahiki.
آية رقم 13
ﯧﯨﯩﯪﯫﯬ
ﯭ
Atapashwa habari binadamu Siku hiyo kwa matendo yake yote, mema na mabaya, aliyoyatanguliza miongoni mwa hayo katika maisha yake na aliyoyachelewesha.
آية رقم 14
ﯮﯯﯰﯱﯲ
ﯳ
Bali binadamu ni hoja iliyo wazi juu ya nafsi yake, yenye kumfuata kwa alichokitenda na alichokiacha,
آية رقم 15
ﯴﯵﯶ
ﯷ
hata kama atakuja na kila udhuru wa kuelezea sababu ya uhalifu wake, hilo halitamfaa.
آية رقم 16
ﯸﯹﯺﯻﯼﯽ
ﯾ
Usitikise, ewe Nabii, ulimi wako kwa Qur’ani wakati wahyi unapoteremka ili ufanye haraka kuihifadhi kwa kuogopa isikuponyoke.
آية رقم 17
ﯿﰀﰁﰂ
ﰃ
Kwani ni juu yetu sisi kuikusanya kwenye kifua chako kisha uisome kwa ulimi wako wakati utakapo. Mjumbe wetu Jibrili akikusomea,
آية رقم 18
ﰄﰅﰆﰇ
ﰈ
basi kisikilize kisomo chake na umpulikize. Kisha isome kama alivyokusomea,
آية رقم 19
ﰉﰊﰋﰌ
ﰍ
kisha ni juu yetu kukuelezea kilichokutatiza kukifahamu katika maana yake na hukumu zake.
آية رقم 20
ﭑﭒﭓﭔ
ﭕ
Mambo sivyo kama mlivyodai, enyi mkusanyiko wa washirikina, kuwa hakuna kufufuliwa wala kulipwa.
آية رقم 21
ﭖﭗ
ﭘ
Bali nyinyi ni watu mnaopenda dunia na pambo lake na mnaacha Akhera na starehe zake.
آية رقم 22
ﭙﭚﭛ
ﭜ
Nyuso za watu wema Siku ya Kiyama zitakuwa ni zenye kung’ara, nzuri na zenye furaha,
آية رقم 23
ﭝﭞﭟ
ﭠ
zitamuona Mola Aliyeziumba na Anayezimiliki, na zitastarehe kwa hilo.
آية رقم 24
ﭡﭢﭣ
ﭤ
Nyuso za watu wabaya Silku ya Kiyama zitakuwa ni zenye kukunjana na kusinyaa,
آية رقم 25
ﭥﭦﭧﭨﭩ
ﭪ
zinatazamia kushukiwa na msiba mkubwa wenye kuvunja.
آية رقم 26
ﭫﭬﭭﭮ
ﭯ
Ni kweli! Pindi roho itakapofika sehemu za juu za kifua,
آية رقم 27
ﭰﭱﭲﭳ
ﭴ
na wakasema baadhi ya waliohudhuria kuwaambia wengine, «Je kuna mtu wa kumzungua na kumpoza kutokana na hali hii aliyonayo?»
آية رقم 28
ﭵﭶﭷ
ﭸ
Na yule ambaye yuko katika hali ya kufa akajua kwamba lile lililomshukia ni kuaga dunia, kwa kuwa anawaona Malaika wa mauti.
آية رقم 29
ﭹﭺﭻ
ﭼ
Na ikashikana shida ya mwisho wa duniani na shida ya mwanzo wa Akhera. Kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka.
آية رقم 30
ﭽﭾﭿﮀ
ﮁ
Watu watapelekwa Siku ya Kiyama: ima Peponi au Motoni.
آية رقم 31
ﮂﮃﮄﮅ
ﮆ
Hakuwa kafiri ni mwenye kumuamini Mtume na Qur’ani, wala hakuwa ni mwenye kumtekelezea Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Swala za faradhi.
آية رقم 32
ﮇﮈﮉ
ﮊ
Lakini aliikanusha Qur’ani na akaipa mgongo Imani,
آية رقم 33
ﮋﮌﮍﮎﮏ
ﮐ
kisha akaenda kwa watu wake akijiona hali ya kujigamba katika kutembea kwake. Basi maangamivu
آية رقم 34
ﮑﮒﮓ
ﮔ
ni yako baada ya maangamivu!
آية رقم 35
ﮕﮖﮗﮘ
ﮙ
Kisha maangamivu ni yako baada ya maangamivu!
آية رقم 36
ﮚﮛﮜﮝﮞ
ﮟ
Je anadhani huyu binadamu anayekanusha kufufuliwa kuwa ataachwa bure: haamrishwi wala hakatazwi, hahesabiwi wala hateswi?
آية رقم 37
ﮠﮡﮢﮣﮤﮥ
ﮦ
Kwani hakuwa binadamu huyu ni tone la manii dhaifu linalotokana na maji matwevu yanayomwagwa na kumiminwa kwenye kizazi,
آية رقم 38
ﮧﮨﮩﮪﮫ
ﮬ
kisha yakawa ni kipande cha damu iliyo kavu. Mwenyezi Mungu Akaliumba kwa uweza Wake na Akazilinganisha sura zake katika umbo la mwili lililo zuri kabisa?
آية رقم 39
ﮭﮮﮯﮰﮱ
ﯓ
Akafanya kutokana na binadamu huyu jinsi mbili: ya kiume na ya kike. Je kwani hakuwa Mola huyo Muumba wa vitu hivyo ni Muweza wa kuwarudisha viumbe wakiwa hai baada ya kutoweka kwao.
آية رقم 40
Ndio! Anaweza. Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, kwa hakika ni Muweza wa hilo.
تقدم القراءة