سورة التكوير

الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس

ترجمة معاني سورة التكوير باللغة السواحلية من كتاب الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس

الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس

آية رقم 1
Pindi jua litakapokunjwa, na mwangaza wake ukaondoka.
آية رقم 2
Na pindi nyota zitakapopuputika na nuru yake ikafutika.
آية رقم 3
Na pindi majabali yatakapoondoshawa kwenye uso wa ardhi yakawa ni vumbi linaloenea.
آية رقم 4
Na pindi ngamia wenye mimba watakapoachwa na kupuuzwa.
آية رقم 5
Na pindi wanyama mwitu watakapokusanywa na kutangamanishwa, ili Mwenyezi Mungu Awape nafasi ya kulipizana wao kwa wao.
آية رقم 6
Na pindi bahari zitakapowashwa moto zikawa ni moto unaowaka.
آية رقم 7
Na pindi nafsi zitakapokutanishwa na mfano wake na sampuli yake.
آية رقم 8
Na pindi mtoto wa kike aliyezikwa akiwa hai atakapoulizwa, Siku ya Kiyama, suala la kumbembeleza na kumkejeli aliyemzika:
آية رقم 9
ni kwa dhambi gani ilikuwa kuzikwa kwake?
آية رقم 10
Na pindi kurasa za matendo zitakapoonyeshwa.
آية رقم 11
Na pindi mbingu zitakapong’olewa na kuondoshwa zilipokuwa.
آية رقم 12
Na pindi Moto utakapowashwa na ukawaka.
آية رقم 13
Na pindi Pepo , Nyumba ya Neema, itakaposongezewa watu wake wachamungu.
آية رقم 14
Litakapotokea hilo, itayakinisha kila nafsi na kujua kile ilichokitanguliza cha kheri au shari.
آية رقم 15
Anaapa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa nyota zinazofichika nuru yake mchana,
آية رقم 16
zinazotembea na zinazoghibu katika anga zake.
آية رقم 17
Na Anaapa kwa usiku unapojitokeza na giza lake.
آية رقم 18
Na kwa asubuhi unapojitokeza mwangaza wake.
آية رقم 19
Hakika Qur’ani ni ujumbe wa mjumbe mtukufu , naye ni Jibrili, amani imshukike.
آية رقم 20
Mwenye nguvu katika kuyapitisha yale anayoamrishwa. Mwenye cheo cha juu kwa Mwenyezi Mungu. Anayesikilizwa na Malaika.
آية رقم 21
Anayeaminiwa juu ya Wahyi anaoteremka nao.
آية رقم 22
Hakuwa Muhammad mnayemjua ni mwendawazimu.
آية رقم 23
Na kwa hakika Muhammad alimuona Jibrili anayemjia na utume katika pambizo kubwa.
آية رقم 25
Wala haikuwa hii Qur’ani ni neno la Shetani aliyefukuzwa na kutolewa kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu. Lakini Qur’ani hii ni maneno ya Mwenyezi Mungu na ni Wahyi wake.
آية رقم 26
Akili zenu zawapeleka wapi katika kukanusha baada ya hoja hizi zilizo wazi na zenye nguvu?
آية رقم 27
Hayakuwa haya isipokuwa ni mawaidha kutoka kwa Mwenyezi Mungu yanapewa watu wote.
تقدم القراءة