وَمَآ أَرۡسَلۡنَا مِن قَبۡلِكَ إِلَّا رِجَالٗا نُّوحِيٓ إِلَيۡهِمۡۖ فَسۡـَٔلُوٓاْ أَهۡلَ ٱلذِّكۡرِ إِن كُنتُمۡ لَا تَعۡلَمُونَ
Nasi hatukuwatuma kabla yako ila watu wanaume tulio wapa Wahyi (Ufunuo). Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Na hatukuwatuma kwa waliotangulia kabla yako, ewe Mtume, isipokuwa Mitume miongoni mwa wanaume, sio Malaika, tunaowaletea wahyi. Na iwapo nyinyi, enyi washirikina wa Kikureshi, hamliamini hilo, basi waulizeni waliopewa vitabu vilivyopita, watawapa habari kwamba Manabii walikuwa ni binadamu, mkiwa hamjui kwamba wao ni binadamu. Aya hii inakusanya kila suala kati ya masuala ya Dini, iwapo mtu hana ujuzi nalo amuulize anayelijua miongoni mwa wanavyuoni waliovama katika elimu.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس