وَلَا تَكُونُواْ كَٱلَّتِي نَقَضَتۡ غَزۡلَهَا مِنۢ بَعۡدِ قُوَّةٍ أَنكَٰثٗا تَتَّخِذُونَ أَيۡمَٰنَكُمۡ دَخَلَۢا بَيۡنَكُمۡ أَن تَكُونَ أُمَّةٌ هِيَ أَرۡبَىٰ مِنۡ أُمَّةٍۚ إِنَّمَا يَبۡلُوكُمُ ٱللَّهُ بِهِۦۚ وَلَيُبَيِّنَنَّ لَكُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ مَا كُنتُمۡ فِيهِ تَخۡتَلِفُونَ
Wala msiwe kama mwanamke anaye uzongoa uzi wake baada ya kwisha usokota ukawa mgumu. Mnavifanya viapo vyenu kuwa ni njia ya kudanganyana baina yenu kwa kuwa ati taifa moja lina nguvu zaidi kuliko jengine? Hakika Mwenyezi Mungu anakujaribuni kwa njia hiyo. Na bila ya shaka atakubainishieni Siku ya Kiyama mliyo kuwa mkikhitalifiana.
Ali Muhsin Al - Swahili translation
Wala msirudi nyuma kwenye ahadi zenu, ukawa mfano wenu ni kama wa mwanamke aliyefuma mfumo akautengeneza vizuri kisha akaufumua, Mnavifanya viapo vyenu mlivyoviapa wakati wa makubaliano kuwa ni udanganyifu kwa mliyopatana naye, mkawa mnazivunja ahadi zenu mnapopata kundi la watu wenye mali kuliko wale mlioahidiana nao. Kwa hakika, Mwenyezi Mungu Anawapa mtihani kwa kuwaamrisha nyinyi mtekeleze ahadi na kuwakataza nyinyi msizivunje. Na ili Apate kuwaeleza, Siku ya Kiyama, yale ambayo mlikuwa mkitafautiana kwayo kuhusu kumuamini Mwenyezi Mungu na kuuamini unabii wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie.
الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس